Nenda
Zako Shetani
Wakati
Yesu anajaribiwa na Shetani mlimani, Majaribu yote kwa namna moja au
nyingine yaliwinda imani yake. Katika moja ya jaribu Yesu alimjibu
hivi Shetani “Nenda
zako Shetani;kwa maana imeandikwa,
msujudie
Bwana Mungu wako, umwabudu Yeye peke Yake”
(Mathayo 4:10).
Hivi
karibuni nilikuwa nikisoma maandiko haya na nikafahamu kwamba,
Shetani unapompinga au unapomfukuza unafanya hivyo kwa andiko.
Unapigana vita vizuri vya imani kwa kusema, “nenda
zako Shetani maana imeandikwa……”.
Katika sehemu hii, tunaangalia kwa mfano vipengele kadhaa katika
maisha uwezavyo kupiga vita vizuri kwa imani, kupitia Neno la unabii
au maandiko. Haya ni baadhi ya matatizo ya kishetani ya kushambulia
imani yako katika maisha.
Woga
Wakati
ushambuliwapo na woga sema, Nenda zako Shetani maana imeandikwa,
nisiogope Yesu ni wa kwanza na wa mwisho (Ufunuo 1:18).
Nenda
zako Shetani, maana imeandikwa, sijapewa Roho ya woga bali ya nguvu
na ya upendo na ya moyo wa kiasi (2 Timotheo 1:7). Nenda zako Shetani
maana imeandikwa kwa Yesu Kristo ninao ujasiri, sio woga wa
kumkaribia Baba kwa Roho Mtakatifu (Waefeso 2:18). Nenda zako
Shetani, sitaogopa maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake walioogopa,
“Jipeni
moyo ni mimi msiogope”
(Mathayo 14:27). Yesu akiwa na mimi sitaogopa chochote. Nenda zako
Shetani, siogopi maisha yangu ya mbele kiuchumi na kimahitaji
yatakuwaje maana imeandikwa “ Msiogope
basi bora ninyi kuliko mashomoro wengi”
Mungu anajua kila kinachotendeka katika maisha yangu zaidi ya
anavyowajua mashamoro (ndege) (Mathayo 10:29-31). Nenda zako Shetani,
sitaogopa yale wanayoyasema
au kunitishia, maana imeandikwa “ msiwaogope
wauwao mwili wasiweze kuiua na roho …”(Mathayo10:28).
Mara
nyingine unaweza kuwa unaamini jambo fulani Mungu kukutendea. Lakini
ghafla mazingira yakabadilika na kuzidi kuwa mabaya. Hii ilitokea kwa
mtoto wa Yairo. Alikuwa anaumwa Yesu alipokuwa anaenda kumponya
wakaja watu wa Yairo na kusema amekufa. Hapa mazingira yalibadilika
ghafla kutoka kuumwa hadi kufa. Bila shaka woga ulimwingia baba yake
na kuuwa imani. Yesu alimwambia “Usiogope
amini tu…”(Marko
5:21 -36). Hata wewe mambo yanapozidi kuwa mabaya kishetani, katika
safari ya imani sema, “Nenda
zako shetani maana imeandikwa usiogope amini tu!”
Mashaka
Katika
hali ya mashaka sema, Nenda zako Shetani, Mungu ni dhahiri sitamwonea
shaka maana imeandikwa, kuna neno gani gumu la kumshinda Bwana?
(Mwanzo 18:13-14). Muda wa Ibrahimu kuzaa ulipita alikuwa mzee. Sara
kimaumbile hakuweza kupata
mtoto lakini kwa Bwana iliwezekana.
Kwa
hiyo sema, Nenda zako Shetani sitalionea shaka Neno la Mungu ni
dhahiri, maana imewandikwa, “ Naliangalia
neno langu nikalitimize”
( Yeremia 1:12).
Maneno
yote niyasemayo kwa kuamini kwa kinywa changu kiroho yanaonwa na
Mungu anayatimiza.
Nenda
zako Shetani, Bwana anayatimiza maneno yake kwangu kwa mkono wake
usio mfupi maana imeandikwa “je
mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona neno langu
litatimizwa kwako au sio “
(Hesabu 11:22-23). Musa na Israeli hawakuona
jinsi gani wangepata
chakula jangwani, lakini kwa mkono wa Bwana alitenda neno lake.
Sema,
Nenda zako Shetani, jambo hili haliwezekani
machoni pangu lakini si machoni pa Mungu hakuna neno gumu
lisilowezekana machoni pake (Zekaria 8:6).
Sema,Nenda
zako Shetani, ahadi za Mungu zinatimia kwangu, Neno lake
linadhihirika maana imeandikwa, “Hakuna
neno lisilowezekana kwa Mungu”
(Luka 1:37).
Sema,
Nenda zako Shetani, Mungu ni mwaminifu yote yanawezekana kwangu,
maana
imeandikwa “hakuna
neno lisilowezekana kwa Mungu”
(Luka 1:37).
Mambo
ya Muhimu Kukumbuka
I-
Bayana
Kabla
ya kupokea jambo kutoka kwa Mungu lazima umwone dhahiri na alichosema
ni dhahiri au bayana. Hii inatokea kwa kusikia Neno, kutafakari,
kulikiri na Roho wa Mungu kulifunua.
II-
Imani
Kumwona
Mungu ni dhahiri na alichosema ni dhahiri kunajenga uhakika wa kitu
alichokisema ambacho kinachotarajiwa kutokea. Uhakika huu hukipokea
sasa na kuwa nacho, hata kama hakijadhihirika moyoni kinakuwa halisi
kabisa. Kwa njia ya udhihiri wa Mungu na neno lake.
III- Kuamini
Uhalisi
ulio ndani unazalisha yatarajiwayo yaonekane kwa kutenda kitu.
Uhalisi huu humsukuma mtu kuomba, kukiri neno kwa ujasiri kinyume na
mazingira, kumshukuru Mungu na kutenda neno. Vita vizuri vya imani
hupiganiwa kwa kuamini na si kwa imani tu. Ikiwa umepokea uponyaji wa
mguu kwa imani na bado unauma, piga vita vizuri vya imani kwa kusema
kitu au kutenda, katika hali ya ustahimilivu na uvumilivu, Amuru uwe
mzima kama ilivyo moyoni.
IV- Yatarajiwayo
Haya
ni yale tuliyoyatazamia kudhihirika katika hali inayoonekana ambayo
tayari tulikuwa nayo kwa imani moyoni. Yarajiwayo yanaonekana kwa
kuitenda imani,kwa kuamini.
Kwa
ujumla Somo hili limeandikwa ili kukusaidia kumtegemea Mungu
katika hitaji lako lolote. Unapoichochea imani yako kwa njia ya
kuyafahamu haya yaliyoandikwa, na kupigana vita
vizuri, bila shaka utaanza kuona mabadiliko katika kumtarajia Mungu
kutimiza ahadi zake kwako. Kwa kifupi ili kuchochea imani yako na
kupata matokeo inabidi ufahamu mambo yafuatayo:
- Uhakika wa imani hujengwa na udhahiri wa Mungu na Neno lake moyoni.
- Imani inayokubalika na Mungu hufanya kazi na Upendo.
- Ufalme wa Mungu ulio ndani yako haushindwi.
- Mungu akiwa upande wako yote yako chini yako.
- Unayo mamlaka ya kuamuru kwa Jina la Yesu.
- Mungu habadiliki alivyowatendea wengine anakutendea.
- Yesu alitoa uhai wake ili ahadi zitimie kwako.
- Mwangalie Mungu awezaye yote kwa Neno lake usiangalie mazingira.
- Tutumie Neno lake la unabii, kupigana.
Ikiwa Somo hili limekusaidia, tafadhali tuandikie ili kushiriki baraka
hiyo pamoja nawe (Tumie Barua Pepe Juu kwenye Bango la Blog hii). Ikiwa unahitaji kumpa Yesu maisha kama Bwana na
Mwokozi wako tafadhali sema sala hii:
Bwana
Mungu nakuomba unisamehe dhambi zangu. Yesu Kristo ingia ndani
yangu, uwe Bwana na Mwokozi kuanzia leo. Kwa njia ya damu yako
nitakase na kwa hiyo nihesabiwe haki. Asante kwa msamaha wa dhambi
na wokovu wako. Amina
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteSehemu Hii ya Mwisho ya Somo Hili la VITA VIZURI VYA IMANI, Kwa Kweli Hata Mimi Mwenyewe Mpaka Sasa Bado Huwa Ninaiona ni Mpya na Yenye NGUVU Zaidi. Hata Sasa Bado Ninajifunza na Inaniwezesha Katika Mambo Mengi ya Kihuduma. NINAKUSIHI USIACHE KUISOMA MPAKA MWISHO NA KUITENDA.
ReplyDeleteUBARIKIWE NA ASANTE KWA KUENDELEA KUJIFUNZA KUPITIA BLOG HII.
Yes Pastor, So Powerful. Thanks.
ReplyDeleteBarikiwa Nawe Pia.