Kumshinda Shetani ni
Kushinda Woga
“Kwa kuwa hamkupokea
tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo
kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba”
(Warumi 8:15)
Zamani, nyakati za
biblia watumwa hawakuruhusiwa kuwaita bwana zao “Aba” yaani baba mpendwa.
Watumwa waliokuwa chini ya mwanamke hawakuruhusiwa kumwita “Imma”. Watumwa na
bwana zao walihusiana kwa misingi ya hofu.
Watoto hawakuwa na hofu waliwaita baba zao “Aba” na mama zao “Imma”, kwa
watumwa haikuwa hivyo.
Nguvu ya Shetani
Roho ya kitumwa ni roho ya dhambi, “…Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” (Yohana 8:34). Roho hii ni chanzo cha woga, au hofu. Adamu alipotenda dhambi tu, alisema yafuyatayo
mbele za Mungu, “…Nilisikia sauti yako
bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi…” (Mwanzo 3:10). Adamu alipotenda
dhambi alikufa, alitengwa na Mungu, hakufa tu!
Bali pia alikuwa mtumwa kwasababu ya roho ya woga, iliyoambatana na
dhambi. Akaanza kumkimbia Mungu!
Mwanzoni alimwona kama Aba, sasa akaanza kumwogopa kama mtumwa! Wanadamu wote
tukageuka kuwa watumwa wa ibilisi kutokana na dhambi ya Adamu, Shetani
akatutawala kwa woga wa mauti, tukawa watumwa.
Yesu Ameondoa Woga
Woga uliingia duniani kwa njia ya Adamu aliyekuwa katika
mwili. Woga unaondoka katika maisha yako kwa Yesu aliyekuja katika mwili. Yesu amemharibu Shetani aliyetutawala kwa
woga wa mauti, Akatuacha huru (Waebrania 2:14). Katika Yesu Mungu amekuwa Baba
yetu, tunamwita Aba kwa kuwa si watumwa tena wa Shetani na dhambi kwa njia ya
Yesu.
WOGA NI MLANGO WA SHETANI KUMWINGIA MTU NA KUMTAWALA. IKIWA UMEMPA YESU MAISHA YAKO, YESU AMEUFUNGA
MLANGO HUO. UKIMTAZAMA YEYE NA KUMTAMKA YEYE KATIKA MAZINGIRA YA WOGA
YANAYOKUZUNGUKA SHETANI HATAPATA NAFASI.
Vyanzo vya Woga
1.
Kuogopa Mambo Yajayo: Kwa mfano
utaishije na uchumi unazidi kuwa mbaya. Unaweza kupata mawazo yanayoongea na
kukuuliza utaishije, bila shaka itakuwa ni Shetani anapandikiza woga ndani
yako, ili kutafuta mlango katika maisha yako. Dawa
ya woga huu ni kujua Yesu ni wa kwanza na wa mwisho, yupo sasa, amekuokoa na
ameshashika na maisha yako yajayo! (Ufunuo 1:18).
2. Kuogopa Kifo: Maandiko
yanasema uhai wetu umefichwa katika Kristo. Shetani hawezi kuupata uhai wako,
labda akaunyang’anye kwa Yesu. Hauishi kwa nafsi yako unaishi kwa njia ya Yesu,
sema na kuwaza hivyo, woga wa kifo utakimbia. Woga huu ni woga wa hatari,
wenyewe ni kifo! Ukiona unaogopa kifo shindana haraka kama unashindana na
Shetani. Kwa kutamka uhai wako ndani ya Yesu (Wakolosai 2:1-3).
3. Kuogopa Kushindwa: Kuogopa kushindwa ni kama vile, kuogopa kuomba kazi kwa kuwa hutaiweza,
kuogopa mtihani kwa kuwa hutafaulu nk.
Kuogopa kushindwa ni kujiandaa kushindwa.
4. Kuogopa Watu: Woga
mwingine mbaya ni kuogopa watu. Kila utakacho kufanya unafikiria watu kwanza,
woga wa namna hii ni mtego, “Kuwaogopa
wanadamu huleta mtego bali amtumainiye Bwana atakuwa salama.” (Mithali
29:25). Woga huu ujapo tamka tumaini lako kwa Mungu zaidi ya watu, utatoka
katika mtego wa Shetani.
5. Kuogopa Yasiyojulikana: Mara nyingine unaweza kujikuta unaogopa kitu kisichojulikana;
Au unaogopa kila kitu; Unaogopa watu, ukipanda basi unaogopa kiti cha basi
kukalia; unaogopa matairi ya basi yatapasuka! itabidi uongee na woga huo kama roho.
Kama kiumbe cha kishetani; kama pepo. Uiamuru itoke kwa jina la Yesu, katika
nafsi yako, pia uambie roho hiyo, hujapewa roho ya woga (2Timoteo 1:7).
Badilisha mfumo wako wa kufikiri,
utabadilisha mfumo wako wa mitazamo, baada ya hapo utajijengea ngome ya
kutoogopa na kuangusha ngome ya woga. Ngome ya woga ni ngome ya kushindwa,
kutoogopa kwa njia ya Yesu ni kushinda.
Wakati wote jenga ngome ya kutoogopa
kwa kusema maneno haya:
Isaya 51:12
Zaburi 118:6
Waebrania 13:5-6
Mathayo 10:28
Mithali 1:33
2Timoteo 1:7
Ufunuo 1:18
UPINGAPO WOGA UNAMPINGA SHETANI
Very True!! Kwa Kweli, Watu Wengi, Wanamtihani katika Swala Hili... Woga/Hofu imeshika Mioyo yao, tena wengine tunaogopa hata visivyoogopeka..aibu hata kuvisema. Nashauri Neno hili tlisambaze kwa Watu Wengi ili Mioyo Mingi Iokolewe! Asante Pastor kwa Hili la Leo Tena. MUNGU Azidi Kukutumia kwa UTUKUFU WAKE!
ReplyDeleteAsante Jimmy, Neno lazima lishinde!
DeleteNimebarikiwa sana kwa neno
ReplyDeleteMuzuri kubarikiwa na kufunuliwa zaidi
ReplyDelete