Matokeo ya Kushukuru
1. SHUKRANI INASIMAMISHA IMANI
Imani hupokea sasa na kuyaona ndani mambo yanayotarajiwa
kuonekana nje baadaye. Shukrani ni tendo la imani linaloonyesha umeshapokea
sasa. Pasipo matendo imani haizai, shukrani ni tendo linaloizalisha imani“Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa
kutoamini bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu” Warumi 4:20
2. SHUKRANI INATAKASA
Luka 17:17 – 19 “Yesu
akajibu, akanena Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? (18) Je!
Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? (19) Akamwambi,
Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”1Timotheo 4:1 – 5
·
Kusafisha
·
Kutenga
Mwenye ukoma alipoenda kushukuru kwa Yesu, alitakasika
kabisa, siyo kupona tu. Tunaposhukuru kwaajili ya chakula kinatakaswa.
Kinatengwa maalum kwaajili ya utukufu wa Mungu.
3. SHUKRANI INAZIDISHA
Yohana 6:1 – 13 “Baada
ya hayo Yesu alikwenda zake ng’ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya
Tiberia.(2)Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu
waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. (3)Naye Yesu akakwea
mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. (4)Na Pasaka, sikukuu
ya Wayahudi, ilikuwa karibu. (5)Basi Yesu alipoinua
macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi
mikate, ili hawa wapate kula? (6)Na hilo alilinena
ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. (7)Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi,
kila mmoja apate kidogo tu. (8)Wanafunzi wake
mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, (9)Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki
wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? (10)Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na
majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. (11)“Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia
walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. (12)Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni
vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. (13)
Basi
wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya
shayiri vilivyowabakia wale waliokula.”
Baada ya Yesu kushukuru mikate na samaki viliongezeka. Unaposhukuru kwa mambo
machache ni rahisi kuongezeka.
4. SHUKRANI INAKUOKOA NA KUNUNG’UNIKA
1Wakorintho 10:1 – 12 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu
walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; (2)wote wakabatizwa wawe wa Musa katika
wingu na katika bahari; (3)wote wakala chakula
kile kile cha roho; (4) Wote wakanywa
kinywaji kilekile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba war oho uliowafuata; na
mwamba ule ulikuwa ni Kristo. (5)Lakini wengi sana
katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. (6)Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi
tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. (7)Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa;
kama ilivyoandikwa, watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. (8)Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya,
wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. (9)Wala tumjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu,
wakaharibiwa na nyoka. (10)Wala msinung’unike,
kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. (11)Basi mambo hayo yote yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano,
yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (12)Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie
asianguke.” Badala ya kunungunika
kwaajili ya mambo yanayokuhusu, shukuru. Shukkrani inaondoa manunguniko na
kukufanya uendelee kumfurahia Mungu.
5. SHUKRANI INAFUFUFA NA KUONDOA HARUFU MBAYA
Yohana 11:38 – 44“Basi
Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa na
pango, na jiwe limewekwa juu yake.
(39)Yesu akasema, liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule
aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. (40)Yesu akamwambia, mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini
utauona utukufu wa Mungu? (41)Basi wakaliondoa
lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa
umenisikia. (42)Nami nalijua ya kuwa
wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria
nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. (43) Naye akiisha
kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. (44)Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na
mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akamwaambia, Mfungueni,
mkamwache aende zake.”. Baada ya Yesu kushukuru Lazaro alifufuka kwa
kuamuru. Msiba uliisha! Maiti iliyoanza kunuka ikaacha. Hali hata ikiwa
imechafuka tushukuru na kutamka mapenzi ya Mungu kwa kuamuru.
6. SHUKRANI NI MAPENZI YA MUNGU
1Wathesalonike 5:18 “shukuru
kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.”
1Yohana 5:14 “Na
huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia.”
Wakolosai 4:2 “Dumuni
sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”. Kuomba
twaomba kwa mapenzi ya Mungu, tunaposhukuru tunafanya mapenzi ya Mungu.
7. SHUKRANI ZINAENENDA NA USAFI WA DHAMIRI
USIACHE KUSHUKURU, UKISHINDWA KUFANYA VYOTE, USISHINDWE KUMSHUKURU MUNGU.
Thank you for the above preachings about the Thanksgiving to our Almighty God.I got a message for the spiritual growth
ReplyDelete