Friday, September 5, 2014

KAZI YA AMANI - I



Amani ni nini?

Kunaweza kuwa na Tafsiri mbalimbali za Neno Amani, hii ni kutokana na weredi na upana wa lugha. Lakini mimi ningepedna nifupishe kwa kusema kuwa amani ni hali ya:-
 
-Utulivu
-Ukimya
-Kutokuwa na mahangaiko au vurugu
-Usalama
-Kutokuwa na uadui

Kwa maana Mungu si wa machafuko, bali wa amani
(1Wakorintho 14:33)
-Mungu si wa vurugu
-Mungu si wa mahangaiko
-Mungu ni wa usalama
-Mungu ni wa upatanisho si uadui
-Mungu ni wa amani

  1. Mazingira ya Kimwili na Kiroho
Wanadamu tuko katika hali mbili kwa wakati mmoja tuko mwilini na rohoni.

Katika hali hizi mbili ili tufanye mambo kwa ufanisi tunahitaji Amani.

  1. Mazingira ya kimwili
Kusipokuwa na amani kimwili ni vigumu kuwa na mafanikio katika yale ufanyayo. Kwa mfano kama wewe ni mfanya biashara kukiwa na vurugu mjini utafunga duka maana hakuna amani.

Hili ni swala la kimwili, lakini hata kiroho usipokuwa na amani utakosa ufanisi wa kufanya jambo.

  1. Mazingira ya Kiroho
Usipokuwa na utulivu wa ndani kiroho si rahisi uwe na mafanikio katika maswala ya kiroho kama vile:
-Kumwamini
-Kumtumikia
-Kumsikia
-Kumwabudu na kumsifu
-Kupata uponyaji wa ndani (vidonda)

Usikose Muendelezo wa Somo hili, Kwani Tutajifunza Mambo Kadhaa kuhusu Amani, kama vile; Nini Chanzo cha Amani? Amani Kabla na Baada ya Anguko, Funguo za Amani, Kazi za Amani, nk.

Lengo ni Kuamsha Ndani Yetu Kiu na Shauku ya Kuitafuta Amani Sahihi katika Maisha Yetu.
 
Mtu anapotubu dhambi zake kupitia Yesu, na kuitegemea kazi ya msalaba na damu ya Yesu ili asamehewe, hupatanishwa na Mungu (HUWA NA AMANI NA MUNGU SI UADUI), pia hatia ya dhambi huondolewa moyoni kwa damu ili awe na utulivu kwa Roho Mtakatifu, utulivu huu ni amani.


No comments:

Post a Comment