MENO
Ikiwa umeokoka, maana ya msingi ya kuokolewa ni kukaa ndani ya Yesu. Neno la Kiyunani, MENO, lilitumika kuonyesha maana ya kukaa au kudumu kuwa ndani ya.
Ili kuweza kuwa na matokeo katika maisha ya wokovu, lazima tujue namna gani tunakaa ndani ya Yesu. Huwa tunaimba, "Nataka kufanana na Yesu moyo wangu" Hii itadhihirika zaidi tunapoelewa maana ya kukaa ndani yake na kukaa humo.
1. MWILI NA DAMU (Yohana 6:56)
Tunakaa ndani yake, naye ndani yetu kwa mwili na damu yake. Ikiwa umempa Yesu maisha yako, Yeye anakaa na wewe na wewe na Yeye kwa njia ya mwili na damu yake. Wakati wa meza ya Bwana si wakati wa kuogopa, ni wakati wa ushirika na muunganiko wa maisha yako na ya Yesu.
2.NENO LA MUNGU (Yohana 15:10)
Yesu alisema, tukishika amri zake tutakaa ndani yake. Huwezi kuzishika ikiwa huzijui. Namna moja ya kuzijua ni kuzisoma, Kisha kuzifikiria na kuzisema. Siku moja katika maombi nilikuwa nikisema kwa kumaanisha Waefeso mlango wa 1. Moyoni mwangu ilikuwa kama Yesu kanitokea! Sikumwona kwa macho, ILA alikuwepo, kwa nini, nilikuwa katika Neno lake. 2 Petro 1:4, andiko hili laonyesha kwa njia ya ahadi za Mungu, tunakuwa washirika wa tabia za Mungu. Neno washirika hapa laweza kumaanisha, tunakaa na Mungu. HII IAMSHE NIA ZETU KUTAFUTA KULIJUA NENO, KAMA KITU CHA THAMANI NA KWA HILO TUKAE NAYE.
3.ROHO MTAKATIFU (1 Yohana 3:24)
Katika andiko hili, sehemu ya kwanza inasisitiza kitu tulichosema hapo juu, kwamba YESU, anakaa na sisi kwa kushika amri zake.
Sehemu ya pili imemtaja Roho Mtakatifu. Ni lazima kumtambua Roho aliye ndani yako, ikiwa unataka kukaa na Yesu. Roho ndani yetu ni Yesu na sisi. Kwa imani onyesha kutambua Yesu yupo nawe kwa kuongea na Roho Mtakatifu. Ongea naye maneno ya kumpenda. Utauona uwepo wa Yesu.
4.IMANI (Warumi 10:17, Waefeso 3:17)
Yesu anakaa na sisi kwa kuliamini Neno lake. Amesema kwa mfano, wote wanaolemewa na mizigo waende kwake(Mathayo 11:28), Kasema Shetani hana kitu kwake (Yohana 14:30) nk. Maneno haya tunapoyasoma, tuyasome kana kwamba ni Yesu mwenyewe yupo mbele yetu anaongea, au angeongea kama angetokea. Mfungwa mmoja wa kikundi cha Hesbola alikuwa akijiuliza Mungu wa kweli ni yupo? Ghafla Yesu alimtokea na kusema, "Mimi ndiye njia na kweli na Uzima..." Yesu alisema naye kama maandiko yasemavyo. Yesu anakaa nasi imani zetu tunapoziweka kwa alichosema. Anatokea kwetu vile vile kama ilivyokuwa kwa wanafunzi.
SOMO HILI BADO NI PANA MUNGU AKITUSAIDIA TUTAENDELEA NALO. ILA AZIMIA KWA HAYA MACHACHE TULIYOJIFUNZA KUANZA KUKAA NA YESU.
No comments:
Post a Comment