Kufunga na Imani
Mara nyingi katika Biblia maombi ya watumishi wa Mungu
yaliambatana na kufunga; 1. Walifunga wakati wa hatari (Esta 4:3), 2.Wakati wa
masikitiko (Nehemia 1:3-4), 3.Wakati wa kutafuta mwongozo wa Mungu (Daniel
9:1-3),
4. Wakati wa kutubu (Yoeli 2:11-12), 5. Wakati wa kumwabudu Mungu (Matendo 13:1-2), 6. Wakati wa kuweka wakfu viongozi (Matendo 14:23), 7 Pia Yesu alifunga kabla hajaanza huduma(Mathayo 4:1-2). Kufunga kunahitajika wakati tunataka kuona mabadiliko makubwa ya kanisa na sisi binafsi, soma Yoeli 2:12-13.
4. Wakati wa kutubu (Yoeli 2:11-12), 5. Wakati wa kumwabudu Mungu (Matendo 13:1-2), 6. Wakati wa kuweka wakfu viongozi (Matendo 14:23), 7 Pia Yesu alifunga kabla hajaanza huduma(Mathayo 4:1-2). Kufunga kunahitajika wakati tunataka kuona mabadiliko makubwa ya kanisa na sisi binafsi, soma Yoeli 2:12-13.
Kufunga kunatuwezesha kujinyenyekeza kwa Mungu na kutukumbusha
kwamba sisi ni dhaifu tunahitaji msaada wake. Kunatuwezesha kuwa na muda mrefu
wa kuomba na kuacha kufikiria chakula na mambo mengine ambayo yanaweza
kutufanya tusimaanishe katika kuomba. Kufunga kunatuwezesha kuwa na nidhamu ya
kula na kuuzuia mwili katika tamaa, kama ya
uzinzi, hasira, uchoyo nk. Ukifunga mara kwa mara ni rahisi kuwa mtoaji (Isaya
58:6-7). Kufunga ni ishara ya nje inayoonyesha tuko tayari kuyatoa maisha yetu
mbele za Mungu, maana chakula hutuwezesha kuishi, hivyo kutokula ni ishara ya
kuutoa uhai wetu. Ukiombea mtu kwa kufunga ni kama
vile umetoa sehemu ya uhai wako kwake.
Biblia kuhusu Yesu inasema, “Akafunga siku arobaini mchana na usiku,
mwisho akaona njaa.” (Mathayo 4:2).
Watu wengi wanaamini kwamba neno hili linalo onyesha kwamba Yesu
alifunga siku arobaini kisha akaona njaa, badala ya kiu, lina ashiria kwamba
Yesu alikunywa maji. Sababu ni kwamba
mtu asipokula muda mrefu kitu cha kwanza anachotamani ni maji sio chakula. Kunywa maji wakati wa kufunga si udhaifu, ni
hekima. Kwa hiyo ni vema ukifunga muda
mrefu unywe maji kwaajili ya afya yako na kulinda heshima ya jina la Yesu
lisitukanwe kwa kutokujua kwako.
Unaweza kutokunywa maji masaa 12,
24, 48 au 72. Baada ya hapo inashauriwa
unywe maji. Hata hivyo kwa ujumla ni vizuri unywe maji wakati wote unapofunga. Kama husikii kunywa maji baada ya siku tatu ni vizuri uwe
na uhakika Mungu amekuongoza kufanya hivyo.
Kufunga na kuomba ni kichocheo cha
imani zetu, ili ziweze kutenda na kusema yasiyowezekana. Yesu alisema, “Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana , amin, nawaambia,
Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa
uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini
namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] (Mathayo 17:20-21). Kwa kifupi katika andiko hili Yesu alisema
kuna namna ya matatizo ambayo hayawezi kutoka mpaka imani zetu zichangamane na
kufunga na kuomba. Kufunga kunaweza kufungulia nguvu ya Mungu katika maisha
yetu na kanisa kwa namna ambayo isingewezekana kwa jinsi nyingine. Sababu ni
kwamba nguvu za Mungu huonekana katika udhaifu. Ukiwa na nguvu kama wewe huna haja ya nguvu ya Mungu, ukiwa huna nguvu
na kumwita Mungu kwa kufunga katika udhaifu huo wa mwili wako Mungu ataonekana.
Maana neema ya Mungu hujidhihirisha katika udhaifu au kutoweza (2Wakorintho
12:9). Kufunga ni ishara ya nje
inayomwambia Mungu, “mimi ni
dhaifu siwezi nakuhitaji kwa imani”.
- Uaanza lini kufunga
- Tenga Siku moja katika wiki ya kuomba na kufunga
- Abudu, Shukuru na kusifu ukiwa umefunga, sio ukiwa na mahitaji tu
No comments:
Post a Comment