Fahamu
ya Kuwa Uko Upande wa Mungu
Ikiwa
umempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako fahamu ya kuwa
Mungu yuko upande wako. Kwasababu yuko upande wako hakuna kitu
kilicho juu yako, kwa kuwa Mungu yupo juu ya vyote. Biblia inasema,
“Basi,
tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu
yetu?”
(Warumi 8:31).
Ili
kudumu katika nguvu na mamlaka ya Mungu aliye ndani yako,
aliyekufanya kuwa mshindi ni muhimu udumu kuwa upande wake.
Usipokuwa upande wake, naye hatakuwa upande
wako,
matokeo ni kuruhusu maadui zako (Shetani, Magojwa nk) kuwa
juu yako.
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kukusaidia kudumu kuwa katika upande wa
Mungu.
- Patana na Nia ya Mungu
Huwezi
kuwa upande wa mtu kama mawazo yako na yake hayapatani. Kama
unahitaji kwenda mahali pamoja naye ni lazima wote muwe na nia ya
kwenda ndipo mtaweza kwenda pamoja. Huwezi kuwa upande wa Mungu na
yeye kuwa upande wako, yaani hamuwezi kutembea pamoja msipopatana
nia, “Je!
Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?”
(Amosi 3:3). Ili uweze kudumu kuwa upande wa Mungu na Mungu awe
upande wako patana naye jinsi uwazavyo. Waza kama atakavyo, waza
kama Neno lake lisemavyo. Usiwaze kama watu wasemavyo, waza kama
Mungu asemavyo. Ukifanya hivi utaweza kuwa na matendo ya Ki-ungu
yatakayomfanya Mungu azidi kuwa upande wako kwa kuwa unatenda kama
awazavyo
na asemavyo.
- Sema kama Mungu Asemavyo
Inakupasa
kusema kama Neno la Mungu lisemavyo, si kama unavyofikiria.
Unapopatwa na tatizo uwe mwangalifu ni jinsi gani unazungumza.
Ukizungumza kinyume na Mungu asemavyo katika maandiko, usitegemee
Mungu kuwa upande wako katika shida hiyo. Ni lazima useme kama
asemavyo, ili awe upande wako na akutetee. Kumwamini Mungu ni
kushawishika kuwa Neno la Mungu ni kweli kama asemavyo, halafu
kulisema kama lisemavyo.
1.Neno
Lililofunuliwa
Ukiwa
ni msomaji wa Biblia Mungu atakupa Neno maalum katika kila tatizo
unalokutana nalo. Atakufunulia andiko litakalo kuwezesha kutoka
katika tatizo hilo. Nakumbuka wakati mmoja nilipatwa na homa kali
sana ya maleria. Roho Mtakatifu alisema nami katika moyo wangu kwa
andiko lifuatalo, “…Mwenyewe
aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.”
(Mathayo 8:17). Kitu nilichokifahamu baada ya andiko hili kufunuliwa
moyoni mwangu ni kwamba, Yesu alichukuwa magonjwa yangu na udhaifu.
Nikajiuliza ikiwa Yesu alichukuwa magojwa na udhaifu wangu, hii homa
ni ya nani? Nikasema moyoni mwangu “Homa hii si yangu ya kwangu
alichukuwa Yesu”, kisha nikaiamuru iondoke kwa jina la Yesu maana
si yangu. Nilipona mara moja baada ya kufanya hivyo. Nikagundua
kuwa Roho wa Mungu akikupa Neno katika matatizo unayokutana nayo Neno
hilo lina uwezo wa kukuokoa kwa kuwa Mungu atakuwa upande wako
kulitimiza.
Mwaka
1998 wakati niko chuoni Tengeru mkoani Arusha, nilishikwa na ugonjwa
wa kifua, ambapo nilikuwa nikikohoa koo linaziba na nashindwa
kupumua, au napumua kwa shida sana. Siku moja usiku kama saa tisa
hivi nilikohoa na sikuweza kupumua vizuri kwa muda! Sauti kama ya
filimbi ilitoka kooni, kiasi cha kuwaamsha baadhi ya wanafunzi
wenzangu toka vyumba vya jirani. Nilijua ninakufa (niliona hali ya
kifo mbele yangu). Nilikuwa nikiweweseka, nashindwa kuvuta hewa,
ilikuwa ni hatari sana! Baada ya muda nilipata nafuu kidogo, ndipo
nikasikia hasira
ndani
yangu
dhidi ya ugonjwa huo.
Nikaenda katika chumba cha maombi. Moyoni mwangu Mungu Roho
Mtakatifu akanipa andiko lisemalo, “…mimi
nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
(Yohana 10:10). Nikaona andikohili ni bayana na nikawa nauhakika
nalo. Nikamuuliza Mungu katika maombi, “je ugonjwa huu ni uzima?”,
halafu nikajijibu mwenyewe katika moyo wangu, “huu sio uzima”,
nikasema “kama sio uzima basi nauamuru kwa jina la Yesu kuanzia leo
usiwepo tena!, kwa kuwa Yesu alikuja niwe na uzima.” Baada ya
kusema hivyo ndio ulikuwa mwisho wa ugonjwa huo, toka siku hiyo
tatizo hilo liliisha. Nikafahamu ya kuwa Mungu alikuwa upande wangu
na kuniponya kwa kuwa nilikuwa upande wake kwa njia ya kulikubali
Neno alilonifunulia na kulitumia kwa neema katika mazingira yangu.
Wakati
fulani nilikuwa nikipata mashambulizi makali katika mawazo yangu.
Mara nyingine nikilala nilitokewa na watu wasio na vichwa, au viumbe
ambavyo sijawahi kuviona, nashindwa kuvielezea kibinadamu. Mara
nyingine vilinitokea vikifanya matendo ya uasherati. Hiki kilikuwa
ni kipindi kigumu sana pengine kuliko vyote katika maisha yangu!,
Ilikuwa ni kipindi cha kujifunza vita vya kiroho. Kwa akili zangu
sikuona uwezekano wowote wa kushinda, ila sikubadili ukiri wangu wa
imani na kutamka kuwa nimeshindwa. Nilikuwa naomba, nafunga,
nakemea, lakini bado tatizo lilikuwepo. Wakati huo ilikuwa ikifika
usiku kwangu ni huzuni, maana nilijua kuwa ni wakati wa hali hizo
mbaya kuanza kunitokea. Katika hali hii ngumu, siku moja sauti
ilisema ndani yangu maneno haya, “Usiogope Damu ya Yesu ina nguvu
kuliko kazi zote za Shetani…usiangalie ukubwa wa tatizo angalia
nguvu ya damu ya Yesu”. Ushuhuda huu ulikuwa dhahiri ndani yangu,
ukanipa uhalisi wa kushinda(Imani). Nilianza kutumia maandiko
mbalimbali yanayohusu damu ya Yesu. Hali hiyo haikuisha mara moja,
lakini nikaanza kuitazama kwa mtazamo tofauti, nikaanza kuiona kuwa
inazidi kuwa ndogo. Imani yangu ikaongezeka nilivyoendelea kukiri
kama Neno la Mungu lisemavyo kuhusu damu ya Yesu. Pole pole nguvu
hizo za upinzani zikaanza kuniachia. Mwishowe nikaweza kumiliki na
kushinda juu ya tatizo hilo. Hali hii mbaya ilikuwa ikinisumbua kwa
muda usiopungua miaka mitatu. Baada ya tatizo hilo kuisha niliumbiwa
moyo wa imani mbele za Mungu na Shetani, isiyoangalia mazingira bali
Neno lake Mungu. Pia ndani yangu kulizaliwa hali ya kuishika ahadi
kwa nguvu na shauku kuu ya Kiungu mpaka ahadi hiyo kudhihirika.
Nilianza kuomba kwa bidii na kumaanisha, pindi hitaji lijitokezapo.
Nilianza kuona vitu vikitokea kama Neno lisemavyo. Hata hivyo
sijiamini mimi binafsi kufanya haya, bali neema ya Mungu na huruma
zake hunisaidia kupita katika majaribu yote na vita.
Nimeandika
shuhuda hizi ili kukutia moyo ujue kuwa Neno la Mungu au ahadi za
Mungu zinaweza kukutoa katika tatizo lako. Mungu akifunua Neno lake
katika maisha yako ni lazima litimie. Kikupasacho kufanya ni
kung’ang’ania ahadi hiyo, yaani kutokubadili ukiri wako na kuwa
na shauku ya ndani itakayokuwezesha kuikiri ahadi kwa ujarisi mkuu.
Hapohapo ukidumu kuishi katika maisha ya upendo. Hatimaye Mungu
atakuwa upande wako na kuitimiza ahadi kwako.
Unapofahamu
Mungu yuko upande wako kwa Neno lake, usibadilishe ukiri wako. Uwe
tayari mbingu na nchi zipite lakini Neno lake lisiache kutimia katika
maisha yako. Uwe na shauku kuu ya kuona Neno lake linatimia.
Usitamke maneno kama, “mbona nimeamini muda mrefu haitokei”
maneno kama haya yatakuangamiza!, badala yake sema, “inawezekana,
inawezekana, inawezekana tu! Bwana yuko ili atimize Neno lake, Mungu
ni wa milele hafungwi na muda”.
Hakika Yuko Upande Wetu! Amen. Thanks Pastor, so Powerful. Na Inafurahisha na Kutia Nguvu Kufahamu ya Kuwa MUNGU Yuko Upande wetu... je Ni Nani Aliye Juu Yetu?? Ni Nini Kitakachotushinda?
ReplyDeleteAMEN
ReplyDelete