Fahamu
Unao Ufalme
Mungu
anatawala kwa mamlaka
yake na nguvu.
Ufalme wake ulipo, nguvu zake, utukufu wake, upendo wake, neema
yake, haki yake, furaha yake pamoja na amani huwepo. Ufalme wa Mungu
ukiwepo yote yanawezekana! maana uko juu ya yote.
Ufalme wa Mungu Unatawala Vitu Vyote
Maandiko
yanasema, “BWANA
ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala
vitu vyote”
(Zaburi 103:19). Kuanzia leo fahamu ya kuwa ufalme wa Mungu uko juu
na unatawala kila kitu.
Hakuna
ugonjwa uliopo juu ya ufalme wa Mungu, hakuna uchawi au mkosi uliyo
juu ya ufalme, kila kitu kiko chini ya ufalme; yaani mamlaka na nguvu
za Mungu.
Ufalme Upo Ndani Yako
Kwa
sababu umemwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako ufalme wake ulio
juu ya kila kitu upo ndani yako. Ndani yako unazo nguvu na mamlaka
ya kutawala kila kitu. Yesu aliwaambia mafarisayo, “…tazama,
ufalme wa Mungu umo ndani yenu”
(Luka 17:21). Kwa kusema hivi alimaanisha ufalme wa Mungu unaweza
kutawala ndani ya mtu na kupitia mtu.
Kuna
mambo kadhaa yanayoweza kukuhakikishia kwamba ufalme wa Mungu uliopo
ndani yako unaweza kutawala vyote kupitia wewe.
Mungu
Mwenye Ufalme Yupo Ndani yako
Biblia
inasema, “Hamjui
ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho
wa Mungu(Mungu)anakaa
ndani yenu?”
(1 Wakorintho 3:16). Mungu ni Mfalme, anao ufalme. Kwa kuwa anakaa ndani yako, utawala wake juu ya dhambi, magonjwa, mashetani na kifo umo ndani yako pia. Unao ufalme unaoshinda ndani yako.
(1 Wakorintho 3:16). Mungu ni Mfalme, anao ufalme. Kwa kuwa anakaa ndani yako, utawala wake juu ya dhambi, magonjwa, mashetani na kifo umo ndani yako pia. Unao ufalme unaoshinda ndani yako.
Roho
Mtakatifu Anakuwezesha Kutawala kwa Ufalme Ndani yako
Maandiko
yanasema, “Maana
ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha
katika
Roho Mtakatifu.”
(Warumi 14:17). Kwa haki furaha na amani katika Roho Mtakatifu wewe
ni mtawala juu ya vyote. Dhambi haikutawali kwa kuwa umehesabiwa
haki, pia ni mtenda haki kwa uwezo wa Roho. Huzuni ya namna yoyote
yakiwemo magonjwa, haikutawali maana u mwenye furaha kwa msaada wa
Roho Mtakatifu. Unayo amani mbele za Mungu kwa damu ya Yesu
iliyokuosha katika Roho wa Kristo. Shetani hawezi kukushitaki tena
hata ukakosa amani, Damu imefanya amani kati yako na Mungu, wewe si
adui wa Mungu damu ya Yesu imekupatanisha na Mungu.
Ufalme
wa Mungu upo Ndani yako kwa Neno lake
Daudi
alisema, “Moyoni
mwangu (ndani
yangu) nimeliweka
neno lako, nisije nikakutenda dhambi.”
(Zaburi 119:11). Neno la Mungu linaweza kukaa ndani yetu kama ufalme
wa Mungu. Ninaamini kuwa ufalme wa Mungu na Neno lake haviwezi
kutenganishwa, kwa kuwa Neno lina mamlaka, nguvu, furaha, amani,
haki, na uwepo wa Mungu. Mtu mwenye Neno la Mungu ndani yake anao
ufalme wa Mungu. Inakupasa kulitafakari Neno mpaka ulione bayana, ili
uhakika uzaliwe utakaobeba yatarajiwayo na kuyazalisha kwa kuamini.
Tawala kwa Kutumia Neno lililo Ndani yako
Neno
la Mungu linao ufalme ulio juu ya yote. Ulitamkapo kwa imani,
unapoliamini ni lazima limiliki na kushinda! Utamkapo Neno kwa
imani unakuwa juu ya kila kitu kinachojaribu kukumiliki, kwa kuwa
unatamka kwa kutumia mamlaka iliyo juu ya mamlaka zote. Utumiapo
Neno juu ya ugonjwa lazima ugonjwa utii na kuondoka kwa kuwa ni
mamlaka iliyo kuu. Ingawa unaweza kuonekana kwamba bado upo, imani
hupokea uponyaji sasa, baada ya hapo huamini kwa kusema kama Mungu
aliye dhahiri asemavyo. Ulitumiapo dhidi ya mapepo lazima yatii kwa
kuwa ni Neno la ufalme ulio juu yao ni Neno la ufalme wa Mungu. Hili
ni Neno lisiloweza kuzuiliwa na mazingira yoyote, ni Neno
lisilozuilika kutenda, maandiko yanasema, “…neno
la Mungu halifungwi.”
(2 Timotheo 2:9).
Malaika
na Ufalme
Malaika
wa Mungu ni watumishi wa ufalme wa Mungu, wanamtumikia Mungu na wale
wanaourithi wokovu (wana wa Mungu), (Waebrania 1:12-13). Malaika
wanasikiliza na kulitenda Neno lake Mungu, wanafanya mapenzi ya
Mungu, maandiko yanasema, “Mhimidini
BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao
neno lake,
Mkiisikiliza
sauti ya neno lake.”
(Zaburi 103:20). Kwasababu malaika wanafanya Neno au mapenzi ya
Mungu, inamaana kwamba wanakutumikia kwa njia ya Neno hilo.
Unapotamka Neno la Mungu lililofunuliwa na Roho Mtakatifu ndani yako,
malaika hulitenda/hulitimiza Neno hilo. Kwa mfano ukisema, “Bwana
Yesu ndiye mlinzi wangu”, kwa neno hilo malaika watakuhudumia na
kukulinda. Uliitapo jina la Yesu likuokoe, kwa mfano toka katika
ajali malaika watakupigania na kukuokoa.
Utamkapo
Neno la Mungu unamiliki kwa nguvu za ufalme wake kwa utendaji wa
malaika zake, haikupasi kuwatukuza na kuwaabudu malaika kwa matendo
yao, bali kumpa Mungu utukufu wote maana wanamwakilisha yeye kwa yale
wayatendayo.
Sasa
umekwisha kufahamu kuwa wewe uko juu ya kila kitu kwa njia ya ufalme
ulioko ndani yako. Achilia nguvu ya ufalme huo kwa njia ya kulitamka
Neno lake kwa imani. Hakuna ugonjwa, kifo, uchawi au laana,
inayoweza kukushinda, unao ufalme ushindao/ utawalao kila kitu;
UFALME HUO, UMO NDANI YAKO, UNATAWALA KUPITIA KINYWA CHAKO.
No comments:
Post a Comment