MANENO NI DARAJA
Mtu anaishi mwilini na rohoni kwa wakati mmoja. Ulimi unamwezesha
kuunganisha mahusiano ya sehemu hizi mbili kwa wakati mmoja. Maneno ni kama daraja la kuvukia toka katika ulimwengu wa roho
kwenda mwilini. Maandiko yanasema, “Roho
ya BWANA ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa
ulimini mwangu.” (2 Samweli 23:2). Hapa tunaona Roho alisema rohoni lakini
neno lile likawa katika mwili yaani ulimi.
Kitu chochote kilichopo rohoni, ili kitokee mwilini njia kubwa ya
kukileta ni maneno. Ikiwa ni kitu kizuri au kibaya. Uzima uko rohoni, unakuja
mwilini na kuonekana kwa maneno. Mauti ipo rohoni inakuja mwilini na kuonekana
kwa maneno. Mungu yupo rohoni ili aonekane, Neno lake husemwa
na Mungu hutokea kwa matendo. Hekima ya Mungu ipo rohoni, ili ionekane inapaswa
isemwe kwa maneno toka moyo wa hekima. Mamlaka ya kutoka pepo ipo rohoni ili
watoke na tuone mwilini tunatamka kwa maneno ya mamlaka. Amani ipo rohoni ili
ionekane mwilini twaisema kati yetu. Mgawanyiko uanzia rohoni, ili roho ya
mgawanyiko itokee mwilini maneno yanahusika kuileta.
Ulimi ni
Usukano
Ulimi ni kama usukani wa gari au merikebu
. Moyo ni kama
dereva aliye shika usikani huo. Mwelekeo
wa gari au merikebu unategemeana na nahodha
anautumiaje usukano. Inategemeana na nia yake anafikiriaje kuhusu
mwelekeo huo. Mwelekeo wa maisha ya mtu
unaendeshwa na moyo wake kwa njia ya
ulimi. Moyo ni nahodha, nahodha huyu anaendesha merikebu ya mwelekeo wa maisha
kwa kutumia usukani uitwao ulimi.
Kuna kitu mtu anakiona moyoni mwake, kutokana na maneno aliyosikia
kisha kutumia usukano yaani ulimi kumpeleka alikoona moyoni. Mioyo yetu ni kiongozi wa maisha yetu.
Tulisikiapo Neno la Mungu tunapata picha, picha hii hutengenezwa kwa njia ya
Neno. Kile tunachokiona moyoni twaanza
kukisema. Ulimi wetu tunautumia kama usukani kutupeleka kule tulikoona moyoni, kisha
maisha yote huelekea sehemu sahihi.
Miaka kadhaa iliyopita nilianza kuona moyoni kwa Neno la Mungu kuwa
mimi ni mwandishi wa vitabu. Hii
ilitokea nilipokuwa kidato cha tano mwaka 1993. Nilianza kusema kwamba
ninaandika vitabu. Nilimshirikisha
mjomba wangu (sasa amelala) Eliot Kaisi
na akanitia moyo kuwa ninaweza.
Niliendelea kusema hivyo mpaka sasa mwelekeo wangu ni kuandika. Moyo
wangu ni nahodha aliona mwelekeo akatumia ulimi kama
usukani na sasa naelekea katika sehemu niliyoona moyoni. Kanuni
hii unaweza kuitumia katika hali yoyote.
Unaona moyoni kwa Neno la Mungu na kusema kinywani kisha mwelekeo hubadilika.
Pia tukumbuke kuwa ili nahodha akate kona hupindisha msukano mara
nyingi sio mara moja tu. Usiseme mara moja au mbili kwa kile unachokiona moyoni
kwa Neno, dumu katika kusema. Pia tuwe
waangalifu, unapozidi kusema kitu kibaya kwa muda, unapodumu kusema mwelekeo wako wote wa maisha
utaenda katika kitu hicho. Inatupasa tuweke mkakati wa kubadili jinsi
tunavyoona ndani katika fikra na mawazo, ili tujue jinsi ya kuzitumia kwa kuona
Neno. Tunajua kuzitumia kwa kuona Neno katika fikra na mawazo yetu, moja ya
mkakati unaoweza kuuweka ni kutafakari na kukariri vifungu vya Biblia au hata
vitabu vya Biblia. Kwa neema ya Mungu nimeweka mkakati wa kusoma, kukariri, na
kutafakari nyaraka nne ikiwemo Waefeso.
Nimemaliza kukariri na kutafakari kitabu hiki mwaka uliopita. Mwaka huu
(2010) ni mwaka wa kutafakari na kukiomba na kukiona moyoni. Hii itaendana na kukitamka ili kibadilishe mwelekeo wa maisha yangu. Nataka kigeuke na kuwa “roho” katika maisha
yangu. Si vema sana
kutoa ushuhuda kama huu lakini naomba nikutie
moyo kwamba huu ni wakati wa kukariri, kutafakari, na kuyaomba maandiko tuyaonayo
moyoni. Baada ya kuyaona tunaanza kuyasema ili yageuze maisha yetu.
Sio lazima uanze kitabu kizima unaweza kuanza na sura moja mfano Yohana
1. Baadaye unaweza kutafakari 1Yohana yote, Yakobo yote au vifungu vyake. Kama
uliweza kukariri mambo mengi shuleni mpaka ukayaona na kuyatumia, si zaidi sana Neno la Mungu. Tuliweke moyoni, tuliseme nalo litaongoza
mwelekeo wa maisha yetu. Biblia inasema, “Tena
angalieni merikebu ingawa ni kubwa kama nini na kuchukuliwa na pepo kali,
zageuzwa na usukani mdogo sana,
kokote anakoazimia kwenda nahodha. Vivyo
hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo
….” (Yakobo 3:4-5) .
Merikebu twaweza kuifananisha na mfumo au mwelekeo wa maisha. Maisha yana misukosuko ambayo ni kama upepo mkali.
Mioyo yetu inapoona Neno la Mungu na kulitumia kupitia ndimi zetu basi
mwelekeo waweza kuwa sahihi pamoja na misukosuko kuwawepo, bila hivyo
tutapoteza mwelekeo.
Ulimi ni
Moto
Kazi moja ya moto ni kuharibu, ni kuteketeza. Ulimi unafananishwa na moto kwa kuwa unaweza
kutoa maneno ya kuharibu kama ni uhusiano
na hata ushirika katika
Kanisa. Moyo mbaya hutumia ulimi
kuharibu mioyo mingine. Moyo ulio na mambo mabaya huyahamishia kwa mtu mwingine
kupitia ulimi. Fumba fumbua! Mioyo mingi
inaweza kuharibika.
Moto ukiwa porini husambaa kwa haraka sana ikiwa kuna upepo. Ila jinsi unavyoanza huanza kidogo. Maneno
mabaya huanza kidogo, lakini yanaweza kusambaa kwa kasi kwa njia ya upepo ambao
ninauita ushawishi wa kishetani. Shetani anaweza kumshawishi mtu katika fikra
aseme kitu “kibaya” kuhusu mwenzake, kama
ni cha kweli au uzushi. Fikra hizi
zikichochewa kwa watu wengi maneno husambaa kama
moto na kuharibu Kanisa zima.
Kitu
adui anachotafuta ni kugawanya Kanisa katika vikundi, kujenga mioyo ya chungu,
kuleta hali ya kudharauliana au watu
kutoaminiana. Hali hii ikiwepo kanisani
ni vigumu kuwa na ushiriki wa Roho Mtakatifu.
Pasipokuwa na ushrika huu Mungu hatatembea
kwa kina kati yetu. Mungu asipotembea kutakuwa na giza, maana Mungu ni Nuru. Giza
likiwepo Shetani atapata nafasi.
Ulimi uliofungamana na moyo mbaya unaweza kulinajisi kanisa zima na kuipa
nafasi mauti, faraka, magonjwa n.k. Pia
ulimi uliofungamana na moyo mzuri unaweza kuliponya Kanisa. Biblia inasema “Nao ulimi ni moto, ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi umewekwa katika viungo
vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa
maumbile nao huwashwa moto na jehanamu” (Yakobo 3 :6).
Very True. MUNGU Atupe Neema Tujue Kuutumia Vyema Ulimi.
ReplyDeleteThanks!
ReplyDelete