Kama tulivyoona kujitambulisha
inatokana na kutambulishwa na maandiko, kisha kujitambua. Huu ni mzunguko ambao unatakiwa uwepo wakati
wote. Lengo lako la kwanza unaposoma
maandiko ya Agano jipya hasa Nyaraka iwe ni kuona Mungu amekutambulishaje. Baada ya hapo anza kutafakari au kufikiria
kwa kurudia rudia jinsi ulivyotambulishwa, pasipo kuona ni vipi utashangaa
unajitambua. Kisha anza kujitambulisha kwa kujitangaza, fanya hivi maisha yote.
Usomapo maandiko lengo liwe ni
kupata maandiko ya maeneo yafuatayo, kisha tengeneza mfumo wako binafsi wa
kujitambua na kujitambulisha kama ulivyotambulishwa:
Mwenye Haki Katika Yesu
Kuzaliwa Mara ya Pili
Kufa, Kufufuka, Kuketishwa na Yesu
Kazi ya Damu ya Yesu
Ukuu wa Yesu
Kuharibiwa kwa Shetani
Kuharibiwa kwa dhambi
Kuharibiwa kwa Magonjwa
Wewe na Kristo
Kristo ni Nani kwako
Wewe ni nani katika Yesu
Na Mengineyo
Unaweza angalia mfumo
nilioonyesha katika kitabu hiki hasa sura mbili za mwisho na kuutumia lakini ni
vema ufanye kwa jinsi yako.
No comments:
Post a Comment