Mwendelezo wa Sura ya VII kutoka wiki iliyopita...
Jitambulishe Mbele ya Mauti
Mauti ndio silaha kubwa au nguvu
kubwa ya Shetani. Kumshinda Shetani na kushinda mauti ni kitu kimoja. Mauti ni
uhai wa Shetani. Mtu yeyote mwenye dhambi akifa na kwenda kuzimu hawezi kutoka
kwa kuwa mauti itamfunga kuzimu. Yesu hakutenda dhambi aliposhuka kuzimu. Mauti
haikuweza kumshika na kumzuia kutoka kuzimu, “24ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwasababu
haikuwezekana ashikwe nao.” (Matendo 2:24).
Alifufuka toka kuzimu akiwa na ‘funguo’, “17Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu,
akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18na aliye hai, nami
nalikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu” (Ufunuo
1:17-18). Yesu anavyoonekana hapa, ni
uwezo wa kudhibiti maamuzi yote ya mauti au kuzimu duniani, hizi ni funguo. Adamu
alipotenda dhambi aliifungulia mauti na kuzimu duniani. Pepo wote na kazi zote za Shetani wana mauti ndani yao. Kama vile mauti
ilivyoshindwa kumzuia Yesu kutoka kuzimu, hata sasa nguvu ya mauti haiwezi
kumzuia Yesu kufanya chochote duniani kupitia kanisa. Yesu duniani ni Kanisa!, “22akavitia
vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwaajili
ya kanisa; ambalo 23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote
katika vyote.” (Waefeso 1:22-23). Pepo yeyote hawezi kulizuia kanisa
kufanya jambo, maana nguvu ya mauti itendayo kazi ndani ya pepo huyo haikumzuia
Yesu kuzimu na Yesu huyo ni kichwa cha kanisa.
Yesu yupo ndani yetu, ni kichwa chetu, kichwa na mwili havitenganishwi, hivyo
kanisa halitazuiwa na mauti au kuzimu duniani kwa njia ya Kristo ( Waefeso
1:23).
Jitambulishe katika ulimwengu wa roho mbele za mauti kwa njia ya Kristo aliye ndani yako. Kwa kuwa mauti ipo ndani ya giza lote ikiwemo
pepo wote, utapata njia ya upenyo kutiisha na kupita maeneo yasiyopitika.
Jitambulishe Mbele ya Magonjwa
Kama tulivyoona mwanzoni
kujitambulisha ni swala la kufanya wakati wote.
Si wakati unaona tatizo tu.
Wakati wote jijengee mfumo wa kujitambulisha mbele za Shetani, mauti, nk
ili kudhihirisha na kuthibitisha kuwa upo juu yake. Dunia imejaa magonjwa jitambulishe
yatakupisha na kukuogoga. Unaweza tumia
maandiko haya: “19Au hamjui ya kuwa mwili
wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala
ninyi si mali yenu wenyewe; 20maana
mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (1 Wakorintho 6:19-20). “17ili litimie lile neno lililonenwa na nabii
Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, na kuyachukua magonjwa yetu.”
(Mathayo 8:17). “24Yeye mwenyewe
alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa
mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”
(1Petro 2:24).
Wakati wote ongea mbele za
magonjwa na kujitambulisha mwili wako ni nyumba ya Roho Mtakatifu na si nyumba
ya magonjwa. Jitambulishe udhaifu wako
ulitwaliwa na Yesu, huo unaoonekana si wa kwako. Jitambulishe katika Yesu huna ugonjwa yeye
aliubeba. Magonjwa mengi ni roho ya
ugonjwa, ukijitambulisha utapata upenyo wa kupona na kuyatiisha.
Jitambulishe Mbele ya Umaskini
Umaskini sio sehemu ya maaisha
yetu katika Yesu Kristo. Kitu chochote
kinachotesa ni sehemu ya laana ya torati, Yesu alifanyika laana ya torati, ili
baraka za Ibrahimu zitufikie. Yesu
alikuwa sadaka ya ukombozi alikuwa sisi ili tuwe yeye, eneo mojawapo
alilotukomboa au kutulipia ni katika umaskini.
Imeandikwa, “9Maana mmejua neema
ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwaajili yenu, ingawa
alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”
(2Wakorintho 8:9). Jitambulishe mbele ya umaskini kuwa Yesu alishakuwa maskini,
hivyo hutakuwa maskini kwa kuwa Yesu amelipia umaskini wako kwa yeye kuwa
maskini badala yako.
Jitambulishe Katika Kristo
Kanisa letu tunaitwa “Word
Drillers” kwa maana ya wachimba Neno.
Vito vya thamani huchimbwa haviko juu ya udongo! Askari mzuri hufanya
“drill” kwa maana ya zoezi la kuweza kutumia silaha vizuri. Mwanafunzi mzuri
naye hufanya “drill” kwa maana ya kujishughulisha akili yake aelewe
masomo. Hata sisi lazima neno la Mungu
tulishibe, tulifanyie zoezi nk. Katika
agano jipya Yesu alikuja kutuingiza ndani yake.
Maandiko ya nyaraka hasa za Paulo, yameeleza sana muunganiko wetu na
Kristo kwa kutumia maneno kama: Ndani yake, kwa yeye, kwa huyo, katika yeye,
pamoja naye nk. Tushike biblia zetu na
kuzisoma, kukopi mistari hiyo na kuitumia kujitambulisha sisi binafsi. Hamna namna nyingine ya kuishi maisha ya
ushindi bila kujitambulisha katika Kristo, na uwezi kujitambulisha, mpaka uone
umetambulishwaje, ujitambue na kuanza kujitambulisha. Ukifanya hivi utajiona kiuthamani katika Yesu
na vitu vibaya utaviona vina kupisha, ila tu tafuta kujitambua wewe ni nani
katika Yesu, kwa kusoma ulivyotambulishwa katika nyaraka, kisha anza kujitambulisha.
Jitambulishe Ulipoketi
Sasa wanadamu walio katika Kristo
Yesu wanaweza kumtawala Shetani,na kuweza kumpinga na kumdhibiti. Yesu alikuja
kama mtu mwingine asiye na dhambi ili kuyarejesha aliyoyapoteza Adamu. Yesu
amefidia maisha yetu kwa njia ya: 1. Kufa msalabani kwaajili ya dhambi zetu au kukataliwa kwetu 2.
Kufufuka kwaajili ya haki au
kukubalika kwetu 3. Kuketishwa mkono wa kuume kwa kushinda kwetu.
Yesu alipopaa na kuketi mkono wa
kuume vitu vifuatavyo vilitokea, katika yeye vitu hivi unavyo pia:
1.
Alikuwa juu ya yote ikiwemo mamlaka zote za kibinadamu na kishetani , “19na ubora wa ukuu wa uweza wake; 20aliotenda
katika Kristo alipomfufua katika wafu; akamweka mkono wake wa kuume katika
ulimwengu wa roho; 21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na
usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule
ujao pia; 22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya
vitu vyote kwaajili ya kanisa; ambalo 23ndilo mwili wake, ukamilifu wake
anayekamilika kwa vyote katika vyote”(Waefeso 1:19-23).
2.
Tuliwekwa juu ya yote pamoja naye, juu ya mamlaka zote za kibinadamu,
kishetani na malaika, “5hata wakati ule tulipokuwa
wafu kwasababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo ; yaani, mmeokolewa kwa neema. 6Akatufufua
pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo
Yesu”(Waefeso 2:5-6). “22Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda
zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.”(1
Petro 3:22).
3.
Alipewa jina kuu kuliko yote na akakeishwa juu ya majina yote “21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka,
na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu,
bali katika ule ujao pia;” (Waefeso 1:21), “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lipitalo kila
jina” (Wafilipi 2:9).
4.
Sisi pia tumepewa pamoja naye jina kuu kuliko yote na tupo juu ya
majina yote, “22akavitia vitu vyote chini
ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwaajili ya kanisa; ambalo
23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
(Waefeso 1:22-23).
5.
Ameonekana mbele za Mungu kwaajili yetu kwa damu yake, “Kwasababu Kristo hakuingia katika patakatifu
palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali
aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni kwa Mungu kwaajili yetu”(Waebrania
9:24). Mbele za Mungu tunakubalika kwa kuwa yupo kwaajili yetu pale, amwonapo
anatuona sisi ndani yake ikiwa tumempa maisha yetu .
6.
Ametupa Roho wake toka mkono wa kuume, “Basi yeye, akiisha kupandishwa, hata mkono wa kuume wa Mungu, na
kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona
sasa na kukisikia” (Matendo 2:33).
7.
Malaika na enzi na nguvu zimeshatiishwa chini yake. Malaika wote na
enzi na nguvu zipo chini ya waamini maana wapo ndani ya Yesu “22Naye
yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu
zikiisha kutiishwa chini yake.”( (1 Petro 3:22).
Endelea Kujifunza Pamoja nami Wiki Ijayo pia ulisha na wengine, Barikiwa
No comments:
Post a Comment