14 “KWA KUWA AMEKAZA KUNIPENDA NITAMWOKOA; NA KUMWEKA PALIPO JUU, KWA KUWA AMENIJUA JINA LANGU” 15 “ATANIITA NAMI NITAMWITIKA NITAKUWA PAMOJA NAYE TAABUNI NITAMWOKOA NA KUMTUKUZA” 16 “KWA SIKU NYINGI NITAMSHIBISHA NAMI NITAMWONYESHA WOKOVU WANGU”
Maandiko haya tuyasomapo kupitia Yesu twaweza kusema, “kwa njia ya Yesu ndani yangu ninampenda Mungu sana ananiokoa na hatari zote na kuniweka palipo juu. Nakuwa juu kazini, shambani, katika lolote nifanyalo kwa njia ya upendo wangu kwa Mungu kupitia Yesu ndani yangu.”
Kwa nini namtaja Yesu hapa, au kwa nini umtaje Yesu? Kwa kuwa huwezi kumpenda Mungu na upendo wako ukakubalika bila Yesu Kristo. Upendo wetu kwa Mungu kwa njia ya Yesu huleta ulinzi na wokovu maeneo yote. Kwa upendo wa Yesu ndani yetu ambao kwa huo tunampenda Baba, tunaomba na kupokea. Mungu anakuwa nasi taabuni anatuokoa na kututukuza.
Si hivyo tu katika agano hili la kulindwa na Mungu anatuongezea siku nyingi, ajali, magonjwa, magaidi, wachawi na kitu chochote hakitakatisha maisha yetu, kwa nini? Tunampenda, tumemjua jina lake, tunamsema kama ngome, kimbilio, kweli na mwaminifu. Tunatiisha nguvu zote za uharibifu kwa ufahamu huu. Kwa kufanya haya kwa neema uhai wetu na umri wetu unaongezeka, adui mwindaji hatakatisha maisha yetu kwa mipango ya gizani tusiyoijua, au ya mchana. Tunahifadhiwa sirini, tunakingwa nayeye.
Katika somo linalofuata tutaangalia mifano ya jinsi tunavyoweza kujiombea bulinzi na usalama katika maisha yetu.
Usitamani kuikosa sehemu hii muhimu ya Somo letu..
No comments:
Post a Comment