ZABURI 91:10-12
10 MABAYA HAYATAKUPATA WEWE, WALA TAUNI HAITAIKARIBIA HEMA YAKO
11 KWA KUWA ATAKUAGIZIA MALAIKA ZAKE WAKULINDE KATIKA NJIA ZAKO ZOTE
12 MIKONONI MWAO WATAKUCHUKUA USIJE UKAJIKWAA MGUU WAKO KATIKA JIWE
Maandiko haya yanaonyesha kwa upana ulinzi wa Malaika. Tunapomwona BWANA kuwa ngome, kimbilio, ngao nakadhalika. Tunaposema hivyo na kutoogopa, Huduma ya Malaika inaachiliwa. Malaika wanaendeshwa na maneno yetu (Zaburi 103:19-20). Tunaposema tupo sirini tumefichwa, yeye ni ngome Malaika huagizwa.
Msitari wa kumi anasema mabaya na tauni hayatatupata: mabaya ni nini? Ni uharibifu. Tauni ni magonjwa. Mara nyingine unapolala sema “Leo sitaota mabaya,” siyo matendo tu hata ndoto au mawazo mabaya hatatupata”. Kumbuka mabaya hayakupati kwa kuwa umetofautishwa katika agano la damu. Mabaya hayakuwapata Israeli kwa damu iliyopakwa katika mti wa mlangoni (Mlangoni), Sasa mabaya hayakupati kwa agano la damu ya mti wa msalaba.
Msitari wa kumi na moja anaanza kwa kusema “kwa kuwa ……”, mabaya hayatupati kwa kuwa atatuangizia malaika zake, watulinde katika njia zetu zote. Magaidi hawatajilipua makanisani mwetu kwa kuwa, atatuagizia malaika watulinde katika njia zetu zote. Wanatulinda hata na amgonjwa.
Msitari wa kumi na mbili umeandikwa mikononi mwao watatuchukua mguu wetu usijikwae katika jiwe. Hizi ni ajali zote za kudhuru mwili kama ni kujichoma na msumari, kuungua, nakadhalika. Malaika wapo wakati wote watuokoe. Kwa sababu ya Agano la damu ya Yesu lililotutofautisha.
ZABURI 91:13
UTAWAKANYAGA SIMBA NA NYOKA, MWANASIMBA NA JOKA UTAWASETA KWA MIGUU.
Simba na nyoka ni ishara za Shetani (soma Luka 10:19, na 1Petro 5:6-8). Kukanyaga ni kukiweka kitu miguuni ni ishara ya kuwa na mamlaka juu ya kitu hicho (Warumi 16:20, Luka 10:19). Kukaa sirini kwake aliye juu, kumsema kama ngao na ngome hutupa uwezo wa kumdhibiti Shetani pande zote, huachilia mamlaka ya kiungu ya kumtiisha. Tunaweza kudhihirisha tuko juu ya kazi zote za kishetani; tukaapo katika Agano na kulisema. Hali hii itatupa hari au ujasiri wa kumpinga adui na kuzitiisha kazi zote. Sema “Mungu ni ngome, ngao, kimbilio, kweli. Malaika zake wanilinda.
Kwa sababu hii Shetani aliye nyoka na simba na kazi zake zote, mitego, magonjwa vimetiishwa chini yangu. Kwa njia ya Yesu Kristo.”
No comments:
Post a Comment