Saturday, September 29, 2018

Maombi ya Ulinzi: TUMETOFAUTISHWA

ZABURI 91:7
IJAPO WATU ELFU WAANGUKA UBAVUNI PAKO. NAAM, KUMI ELFU MKONO
WAKO WA KUUME! HATA HIVYO HAUTAKUKARIBIA WEWE.


Maneno ya andiko hili ni maneno yanaoonyeshwa kutofautishwa.
Musa aliona kutofautishwa kwa wana wa Israeli na wa Misri.
Damu iliwekwa juu ya miimo ya milango ya Waisraeli ikawatofautisha na wa
Misri hawakupigwa na Malaika (Kutoka 12:13).
Damu ndiyo iliyokuwa msingi wa agano wa kuwatofautisha.
Walitofautishwa kwa agano la damu.
Kutoka 8:22
Inzi walioisumbua Misri kama pigo hawakuwepo Gosheni kwa Waisraeli ingawa
ilikuwa ni hapo hapo.
Mvua ya mawe iliyopiga Misri haikupiga Gosheni (Kutoka 9:26).
Hii inaonesha kwamba walitofautishwa. Nini kiliwatofautisha?
Walikuwa na Agano na Mungu.


Andiko hili linaonyesha kwamba hata kama kuna vitu vinaathiri dunia ambavyo vinatisha,
tumetofautishwa na dunia havitatupata. Tuonapo tatizo linawapata watu wote tuwaze na
kusema moyoni mfano “Japo watu elfu na makumi elfu wanakosa kazi,
kukosa kazi hakutanipata mimi.  Siko duniani nimo ndani ya Yesu nimetofautishwa”


Safina iliwatofautisha Nuhu na watoto wake na wake zao.
Walipona kwa kuwa ndani ya Safina.
Sasa tunapona na kutoautishwa kwa kuwa ndani ya Yesu.
Kujiona na kujisema kuwa uko tofauti na dunia na yaliyo duniani ni njia ya kuanza kushi
kimiujiza na kuokolewa na hatari. Taja kitu sema, “Ingawa watu maelfu na makumi elfu
wanapata ajali na kufa na kuvunjika haita nipata mimi katika Yesu Kristo”.


ZABURI 91:8 – 9
8 “ILA KWA MACHO YAKO UTATAZAMA,
NA KUYAONA MALIPO YA WASIO HAKI.”


Maandiko yanasema tusimlipe mtu ovu kwa ovu. (1Petro 3:9). Mungu ndiye alipaye kisasi
(Warumi 12:19).
Tuendeleapo kumwona Mungu kuwa ni ngome, kimbilio, ngao na kadhalika
na kumsema hivyo, maadui zetu, yeye atashughulika nao sisi haturuhusiwi.
Baadaye tutaona kisasi chake mbele za macho yetu.
Sisi tukazane na kujiona salama kwa BWANA, tusijishughulishe na watu,
yeye atashughulika nao. Imba Bwana ni ngome, kimbilio, ngao, furahi na kuimba wakati
wote mengine mwachie yeye.


9 “KWA KUWA BWANA NDIWE KIMBILIO LANGU; UMEMFANYA ALIYE JUU
KUWA MAKAO YAKO.”
Ukweli wa andiko hili pia unaendana na msitari wa 1,2 na wa tatu.

No comments:

Post a Comment