Wednesday, September 5, 2018

Maombi ya Ulinzi: Anatuokoa

MAOMBI YA ULINZI
Mwendelezo wa Somo la Maombi ya Ulinzi....

ANATUOKOA
ZABURI 91:3
MAANA YEYE ATAKUOKOA NA MTEGO WA MWINDAJI NA KATIKA TAUNI IHARIBUYO


ATAKUOKOA
Neno lililotumika ‘Kuokoa’ toka mtego wa mwindaji hapa ni “deliver” kwa kiingereza.
Neno hili pia limetumika Mathayo 6:13, “… utuokoe na yule mwovu” kwa Kiyunani
Neno hili ni Ryomai, ambalo maana yake ni kutoa kitu katika hatari, kuvuta kitu haraka kwako
kutoka mahali. Mfano mtoto anataka kuvuka barabara ukivuta haraka kwako umemwokoa
kwa maana ya neno hili. Paulo alitumia neno hili (ryomai) alipoandika,
“Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wa mbinguni ……”
(2Timotheo 4:18).


Hapa ametajwa mwindaji, lakini kutokana na Mathayo 6:13 ametajwa shetani, basi twaweza
kusema, mwindaji anayetajwa hapa ni shetani ategaye mitego ya mauti.


MTEGO
Neno mtego katika andiko hili ni“Snare” kwa lugha ya kiingereza.
Katika 2Timotheo 2:26 imeandikwa, “Wapate tena fahamu zao,
na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye,
hata kuyafanya mapenzi yake.” Katika lugha ya Kiyunani neno Pagos limetumika
hapa likimaanisha mtego. Lugha ya picha ya neno hili maana yake ni
mkakati uliofichika wa kukamata kitu. Ni jaribu la kumkamata mtu katika maangamizi.
Mungu katika Yesu Kristo anatuokoa na kila kitu cha kishetani kilichojificha ambacho
kusudi lake kitukamate na kutukosesha uzima wa milele.
Sema hivyo, taja majaribu ya tamaa ya mwili, macho na kiburi cha uzima.
Mikakati yoyote ya shetani maeneo hayo sema anakuokoa itakuwa hivyo.


TAUNI IHARIBUYO
Tauni ni ugonjwa unaosambaa na kuambukiza. Tauni inayotajwa hapa ni ugonjwa wa
kishetani unaoharibu. Neno iharibuyo hapa limefanana na Ufunuo 16:2,
kwa Kiyunani neno hili ni Kakos, ni kitu kibaya cha kuharibu, hasa mwili.
Mungu anakutoa haraka anakuvuta kwake toka hatari ya mtego wa kishetani wa kukufanya
umkosee, na magonjwa ya uharibifu wa mwili, sema hivyo.


ZABURI 91:4
KWA MANYOYA YAKE ATAKUFUNIKA CHINI YA MBAWA ZAKE UTAPATA KIMBILIO.
UAMINIFU WAKE NI NGAO NA KIGAO.


Andiko hili yaliyomo ndani yake kwa karibu yanafanan na msitari wa 1 na wa 2.
Ila sehemu ya pili ya uaminifu wake tutaitazama.

UAMINIFU WAKE NI NGAO NA KIGAO
Neno uaminifu wake hapa katika tafsiri ya KJV, kwa kiingereza ni “Ukweli”,
“Ukweli wake ni ngao (shield) na kigao (buckler)”


PICHA NGAO
Ngao ni kitu au kinga kubwa mfano Wamaasai ngao zao ni kubwa.
Akiiweka chini inaweza kufika hata kifuani, katika Waefeso 6, ngao iliyotajwa ni kubwa
askari akiishika ilikuwa inaweza kuzuia au kukinga karibu mwili mzima.
Ingeweza kupinga mishale, panga, mawe nk. Umbo lake lilifanana na pembe tatu.
Kigao ni kinga pia ila ilikuwa na umbo la mviringo.
Ilitumika Zaidi katika mapigano ya mapanga, na haikuzuia mwili wote.
PICHA KIGAO
Uaminifu (Ukweli) wa Mung,  Neno lake kwetu ni kinga! Unaweza kusema
“Kinga yangu dhidi ya mashambulizi yote ya kishetani ni
Ukweli wa Mungu na Neno lake ninalolisema.”
Chochote unachokiona kinakushambulia au kinatisha Kinga yake ni ukweli wa Kiungu.
Ufikirie huo, useme huo na kamwe hutaangamizwa.

2 comments: