Wednesday, August 29, 2018

Maombi ya Ulinzi: Tunasema

MAOMBI YA ULINZI
Mwendelezo wa Somo la Maombi ya Ulinzi....
TUNASEMA
ZABURI 91:2
“NITASEMA BWANA NDIYE KIMBILIO LANGU NA NGOME YANGU,
MUNGU WANGU NITAKAEMTUMAINI”


KIMBILIO
Zamani Agano la Kale kulikuwa na miji ya makimbilio, baadhi ya watu waliofanya makosa
yastahiliyo kuuawa, waliweza kukimbilila katika miji hiyo na kuwa salama (Hesabu 35:6)
Hebu ingia moyoni mwa mtu anayetaka kuuawa na mbele yake anaona mji wa makimbilio,
nini anakuwa nacho moyoni? Anautegemea ule mji tu! Anautumania wenyewe.
Ndivyo hivyo kwetu tunamwona Bwana peke yake ndiye mahali pa kuponea.
Ingia moyoni mwa Petro alipokuwa anazama, aliona pa kuponea ni katika Bwana tu!         
(Mathayo 14:29-30). Bwana Yesu ndiye kimbilio letu, ndio mji wa kuponea kwetu.
Inatupasa tuseme hivyo. Andiko hili linaanza kwa kusema “Nitasema”.
Hivyo tuseme hivyo na itakuwa hivyo.


NGOME
Ngome ni ukuta. Ukuta unaokinga. (Isaya 25:12). Mtu aliyezungushia nyumba yake
ukuta wasiwasi haupo sana kwamba kuna mtu anaweza kuingia.
Moyoni mwake anautumainia ukuta huo.


Andiko hili (Zaburi 91:2) Linaonyesha matumaini yetu ni katika Bwana,
aliye kimbilio, mji wa kuponea, lakini pia aliye kinga. Bwana ni mahali petu pa kuponea,
Bwana ni mahali petu pa kukingwa! Sema hivyo itakuwa hivyo, ona hivyo woga utakimbia.


MUNGU NITAKAE MTUMAINI
Matumaini yetu kwamba tuko salama hatuna madhara ni pale tuonapo Bwana ni pa kuponea
kwetu na kinga yetu, katika Bwana:

  1. Tupo ndani yake (tunaketi)
  2. Tunadumu ndani yake (tunakaa)
  3. Tumefichwa sirini (tunazungukwa)
  4. Tuko uvulini (Hatuonekani)
  5. Tunalo kimbilio (Tunapo pa kuponea)
  6. Tumo ngomeni (Tumekingwa)

Yaseme mambo haya katika Yesu Kristo, sema Nimeketi ndani ya Yesu, ninadumu hapo,
nazungukwa na Mungu, sionekani na adui, ninapo pa kuponea, nimekingwa na ngome.
Sema mpaka uone ndani yako ukweli huu.

No comments:

Post a Comment