MAOMBI YA ULINZI
Mwendelezo wa Somo la Maombi ya Ulinzi....
NGUZO NNE ZA ULINZI
Katika kitabu hiki kuna mambo kadhaa tunajifunza kuhusu maombi ya ulinzi kwa
kutumia Zaburi 91. Nimeona ni vema ingawa tunaipitia Zaburi yote, kwanza kuonyesha
maeneo manne unayoweza yatumia wakati wote kujiombea ulinzi. Nimeandika hapa
mwanzoni kwa kuonyesha umuhimu wake.
kutumia Zaburi 91. Nimeona ni vema ingawa tunaipitia Zaburi yote, kwanza kuonyesha
maeneo manne unayoweza yatumia wakati wote kujiombea ulinzi. Nimeandika hapa
mwanzoni kwa kuonyesha umuhimu wake.
Ulinzi wa Mungu ni wa maeneo yote, mawazo yetu, miili yetu, nk, maeneo yote,
nguzo hizi nne twaweza zitumia kwa imani.
nguzo hizi nne twaweza zitumia kwa imani.
NENO
91:4
Katika zaburi hii msitari wan ne, imeandikwa uaminifu wake Mungu ni ngao na kigao.
Katika tafsiri za Kiingereza neno hili uaminifu ni kweli. Kweli yake ni ngao na kigao.
Kweli ni nini, Yohana 17:17 inasema Neno la Mungu ni kweli.
Ulinzi wa kiungu hutokea tunapotumia neno lake maishani mwetu.
Kipengele hiki tutakipitia hapo mbele katika kitabu hiki. Neno linatutenga na uharibifu.
DAMU
91:10
Katika kutoka 12:13, Mungu alisema akiona damu atapita juu yao uuaji wa malaika wa
mauti au tauni usingewapata. Hapa msitari wa kumi inasema mabaya hayatakupata na
tauni haitaikaribia nyumba au hema yako au makao yako. Wakati wapo Misri wana wa
Israeli, mauti haikukaribia nyumba zao kwasababu ya damu ya kondoo wa pasaka.
Sasa mauti haitukaribii, na mabaya hayaji maishani mwetu kwa damu ya Mwanakondoo
Yesu Kristo. Sisi ni nyumba ya Roho Mtakatifu, juu yetu tuna damu ya Yesu.
Wakati wote tuiseme damu katika ushuhuda wetu, kwa kile ambacho damu
imefanya maishani yetu (Ufunuo 12:11).
imefanya maishani yetu (Ufunuo 12:11).
MALAIKA
91:11-12
Katika njia zetu zote malaika wapo nasi kutulinda. Hutulinda kwa kutumia maneno yetu
tunayosema kwa njia ya neno la Mungu (Zaburi 103:19-20). Wao wanasubiri wakati wote
kutuhudumia katika ulinzi kwa yale tusemayo. Ni wahudumu wetu maana tumempa
Yesu maisha yetu na kuwa warithi wa wokovu (Waebrania 1:14).
Mara nyingine watamke kwa kusema, “Kwa jina la Yesu malaika mnaachiliwa
katika ulinzi eneo hili au safari hi ink”. Zaburi 34:7, inasema malaika huwazunguka
wamchao na kuwaokoa, wamchao ni watu wa Mungu.

JINA
91:14
Agano la kale limetaja jina la Bwana kuwa ni ngome (Mithali 18:10).
Ngome ni kitu kinachozunguka na kulinda. Jina la Yesu Agano jipya ni ngome
inayotuzunguka na kutulinda. Kulindwa kunaendana na kutunzwa na kutopotea,
Yesu alisema, “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa,
nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu ili
andiko litimie.” (Yohana17:12).

MAMBO HAYA MANNE YASEME WAKATI WOTE, HASA UNAPOAMKA
ASUBUHI NA KUIANZA SIKU. SEMA KWA WATOTO WAKO,
MUME AU MKE WAKO, KAZI YAKO, FIKRA ZAKO ZISISHAMBULIWE,
HUDUMA NK. NI NGUZO NNE ZA ULINZI MAENEO YOTE.
ASUBUHI NA KUIANZA SIKU. SEMA KWA WATOTO WAKO,
MUME AU MKE WAKO, KAZI YAKO, FIKRA ZAKO ZISISHAMBULIWE,
HUDUMA NK. NI NGUZO NNE ZA ULINZI MAENEO YOTE.
Usikose Muendelezo wa Somo hili wiki Ijayo....
No comments:
Post a Comment