Kusudi la miili yetu ni kumwabudu Mungu. Shetani anataka aharibu miili yetu isiwe na sifa ya kuabudu. Kitu akitumiacho ni dhambi ya uzinzi.
Uzinzi ni nini? Ni kufanya tendo la kujamiiana mwanaume na mwanamke bila kuwa mume na mke. Ikiwa ni kabla mtu hajaoa au kuolewa, pia kufanya na mume au mke wa mtu mwingine. Mara nyingi uzinzi hutamkwa kwa mtu mume au mke aliyetoka nje ya ndoa yake. Tendo hili la kukutana mwanamke na mwanamke linafanyika katika ndoa tu, nje ya ndoa au kabla ya ndoa ni uzinzi (1 Wakorintho 7:1-2).
Uasherati ni nini? Uasherati ni matendo yote ya kujamiiana au kuwasha tamaa, ikiwemo uzinzi. Uasherati ni neno pana zaidi ya uzinzi.Mara kwa mara hutumika kwa mwanamke na mwanaume kutembea kabla ya kuoana. Lakini haiishii hapa tu ina maana pana zaidi. Mambo ya Walawi 20:10-21, imeonyesha matendo ya uasherati, uzinzi ukiwemo ndani yake. Soma maandiko haya.
MALAYA WA KIUME
Maandiko yanasema, "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike, Waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi..." (1Wakorintho 6:9).
Pornos: Neno waasherati katika andiko hili ni "pornos" katika lugha ya Kiyunani. Tafsiri yake ya msingi ni malaya wa kiume, watendao matendo ya kujamiiana kwa ujumla yake, yasiyo sawa na utaratibu wa Mungu.
Moichos: Neno hili "moichos" Lina maana ya mwanaume atembeaye na mke asiye wake.
Kwa maneno haya mawili utagundua wanaume wanahusika moja kwa moja na kuondoa uasherati na uzinzi au kuuendeleza. Wanawake nao wanahusika ila ni katika ushawishi. Wanaume wanahusika na maamuzi ya kufanya au kutofanya. Kama vile wanaume walivyo vichwa katika ndoa ndivyo ilivyo katika dhambi hizi. Kwa kusema hivi haina maana wanawake hawana hatia.
KUKIRI NA KUACHA
Dhambi ya uzinzi baada ya kuikiri kwa kutubu, hatua ya pili ni kuiacha. Watu wengi huungama uzinzi ila hawachukui hatua za kuuacha. Baada ya kukiri fanya vitu vya kuuacha: Mfano usiwasiliane na mliyezini naye, futa namba ya simu, jitenge naye katika nafsi kwa kumwondoa kwa jina la Yesu nk.
NGAZI ZA UZINZI
Ili mtu afunguke kabisa katika uzinzi, ni vizuri kujua unamhudumia katika ngazi ipi. Kuna ngazi kadhaa.
1.Uzinzi ni kuasi Sheria (Transgress)
Mtu azinie amekiuka sheria ya Mungu isemayo usizini. Hapa inampasa kukiri na kuomba rehema.
2.Uzinzi ni Machukizo (Iniquity)
Uzinzi unaweza kuwa si kuvunja sheria tu, bali tabia inayojirudia. Hii ni machukizo. Huyu anaitaji si kutubu tu, Bali kujenga mfumo na tabia ya kujirudia itakayo mzoeza kuishi maisha mengine. Pia tabia hii ya kujirudia inaweza kuwa ni matendo wa mwili.
3.Uzinzi ni roho (spirit)
Uzinzi unaweza kuwa pepo lililomwingia mtu baada ya kuzini au kubakwa. Roho hii kifungo chake huvunjwa, na pepo kupingwa na kutolewa
4.Uzinzi ni Muunganiko wa Nafsi
Mtu azinipo hujiunganisha nafsi na aliyezini naye kwa njia ya damu zao kuungana. Ni lazima kujitenga naye kwa kutubu na damu ya Yesu
No comments:
Post a Comment