Wednesday, October 19, 2016

Huduma Kuu ya Yesu-KUFUNDISHA

YESU ALIFUNDISHA ZAIDI YA KAZI NYINGINE YEYOTE ALIYOFANYA.

*Kazi ya Yesu kuu na ya kwanza ilikuwa ni kufundisha.

*Kazi yake kuu na ya kwanza sasa ni kufundisha.

*Kufundisha ni moja ya tendo la ajabu la Yesu: Luka 19:37.


1. Yesu alifundisha kabla ya huduma nyingine yoyote (Mathayo 4:23, 9:35).

2.Kazi kuu zinatanguliwa na kufundisha au kujifunza (Marko 6:2).

3.Kufundisha ni kuchunga (Marko6:34)

4.Kufundisha kwa Yesu kuliendana na mamlaka yake (Mt21:23, Marko 1:22)

5. Alipoona hawaamini alifundisha kujenga imani (Marko 6:6).

6.Alipokuwa akifundisha uweza ulidhihirika
(Luka 5:17).

7. Luka 23:5, mafundisho yanachochea, yanataharakisha jambo kufanyika. Ikiwa inahitajika jambo lifanyike watu wakifundishwa huchochewa.

8.Marko 2:13, walipomsonga aliwafundisha.

9.Akawafundisha tena, Marko 10:1. Kufundisha jambo kunahitajika tena na tena.

10. Alifundisha kila siku,( Luka 19:47-48)


UMUHIMU WA KUJIFUNZA
1.Kubadilika mtazamo
2.Mungu kudhubiti maisha yako kama mchungaji
3. Maarifa na hekima
4.Kukarabati imani
5.Kuchochewa kutenda mema
USIACHE KUFUNDISHA NENO, USIACHE KUJIFUNZA

No comments:

Post a Comment