YOHANA 10:17
Yesu aliutoa uhai wake msalabani alipokufa, akautwaa alipofufuka. Ameonyesha ukuu wake kwa uwezo wa kutoa uhai wake ili autwae tena!
Alitoa uhai wake ayabebe na kuyalipia maisha yetu. Aliutwaa uhai wake kwa kufufuka tuyapate maisha yake.
Jina lake linaweza kudhihirisha haya katika maisha yetu. Kwa jina la Yesu unaweza kuyakataa maisha yako yenye dhambi kwa kuwa Yesu alifanyika dhambi zako, unaweza kuyakataa magonjwa kwa kuwa alibeba magonjwa yako. Baada ya hapo kwa jina hilo hilo ukatamka uponyaji utokao kwake na msamaha utokao kwake.
Kwa jina la Yesu unaacha yaliyo yako na kuyapata yaliyo yake.
No comments:
Post a Comment