Tuesday, August 16, 2016

JINA LA YESU-8

MATENDO 19:13-16

Jina la Yesu ni jina la kimahusiano. Kabla hujalitumia lazima uwe na uhusiano na mwenye jina. Katika maandiko hayo hapo juu kulikuwa na watoto wa Skewa, walijaribu kutoa pepo kwa jina la Yesu wakati hawana uhusiano na Yesu! Walitaka kulitoa pepo kwa kuiga, walimwona Paulo anatoa pepo nao wakaiga. Jina la Yesu nguvu yake ni kuwa na uhusiano naye. Kwanza kabisa ni kumpokea maishani mwako.


Uhusiano na Yesu unaanza ukimpa maisha. Baada ya hapo uhusiano huleta; Ushirika. Ushirika unajusisha mambo kama vile; kila siku kuomba, kusoma neno lake, kumtafakari, kumwimbia, kujitenga na uovu nk. Ushirika huimarisha uhusiano, katika hali hii utumiapo jina lake ni rahisi kuwa na imani nalo, maana kwa uhusiano na ushirika na mwenye jina utakuwa unamuelewa vizuri yukoje. Ukiwa na ushirika na mtu unamjua. Ukiwa na ushirika na Yesu kwa kuwa mnahusiana utazidi kumjua. Imani yako itakuwa ina nguvu ndani yake, hatimaye utakuwa na imani kuu katika jina lake hata mashetani watakufahamu kama walivyosema walikuwa wanamfahamu Paulo.

No comments:

Post a Comment