MATENDO 9:15
Yesu alipokuwa anamwita Sauli, ambaye ni Paulo, alisema amemwita kuwa chombo na atalibeba jina lake kwa Mataifa. Kulibeba jina hapa limetumika neno la Kiyunani "Bastazo" Ambalo linafanana na kubeba kitu chenye uzito. Jina la Yesu ni kitu halisi kinacho bebeka.
Leo fahamu ya kuwa ulipookoka umebeba jina la Yesu. Linao uzito wa uwezo wa Mungu, linao uzito wa mwangaza wa Mungu. Na wewe limekufanya mzito! hauwezi kuyumbishwa na pepo au chochote, umejazwa na kujaa jina la Yesu. Sema hivyo, itadhihirika hivyo.
Yesu alisema ametupa amri ya kukanyaga nyoka na nge (Luka 10:19). Neno la Kiyunani "Pateo" Tafsiri yake ni kukanyaga kwa maana ya kuponda au kusigina. Huwezi kuponda kitu bila kutumia shinikizo kubwa juu yake. Neno amri (exousia) Katika andiko hili tafsiri yake ni mamlaka. Mamlaka ni jina la Yesu.
Mimi ninaamini unapozungumza kuhusu mamlaka ya Mungu na jina la Yesu ni kitu kimoja. Hivyo Yesu angeweza kusema, "Tazama nawapa jina mlibebe, ili muweze kuponda kwa kutumia ukuu na uzito wake; kuweza kusigina nyoka na nge na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru"
Mpendwa, ndani yako umebeba jina la Yesu, wewe si mwepesi ni mzito kiroho! Unapokanyaga nyoka na nge wanapondeka pondeka kabisa.
No comments:
Post a Comment