Saturday, August 13, 2016

JINA LA YESU-6

WAKOLOSAI 3:17


Jina katika lugha ya Kiyunani "Onoma" Linaonyesha mamlaka na tabia ya mwenye nalo.

Unapotumia jina la Yesu, unavaa mamlaka yake na tabia yake. Unaposema leo naenda kazini, nitafanya kazi kwa jina la Yesu ni sawa na kusema nitafanya kazi kwa mamlaka na tabia ya Yesu (Mfano: Tabia ya upendo, amani nk).


Maandiko yanasema kama yeye alivyo ndivyo na sisi tulivyo ulimwenguni humu (1Yohana 4:17), Kama alivyo kimamlaka na kitabia ndivyo tulivyo! Ni kivipi? Kwa njia ya jina lake.
Tunapolitumia tunakuwa kama yeye eneo husika. Kama kazini wanakuchukia ingia kwa jina la Yesu, hutaenda na tabia ya kisasi, utaenda na tabia ya Yesu ya amani. Kama kuna ushirikina ingia kwa jina la Yesu, hapa utakuwa umeingia kwa mamlaka yake inayotiisha kila kitu!


Nimetoa mfano wa kazi, lakinj waweza fanya hivi katika huduma, shuleni nk.

No comments:

Post a Comment