Monday, August 8, 2016

JINA LA YESU-1

MATHAYO 9:20-21, MATENDO 3:16

Nimejifunza mbele za Mungu, mwanamke aliyekuwa anatoka damu alishika vazi la Yesu/Alimshika Yesu nguvu zikamtoka Yesu na kumponya. Kumshika huku ni kumwamini. Leo Yesu hatuko naye kimwili tuko naye kwa jina lake. Imani katika jina lake ilimtia nguvu kiwete akatembea, nguvu hii ni ileile iliyomponya mwanamke toka kwa Yesu. Sasa nguvu hiyo tunaipata kwa jina lake kama ilivyotokea kwa kiwete. Jina la Yesu ni Yesu katikati yetu. Kama vile Musa alikuwa na fimbo Mungu akaonekana, sisi tunalo jina la Yesu, Yesu anaonekana bila maswali!

No comments:

Post a Comment