Saturday, August 6, 2016

IMANI NA MSALABA

NIMEYAPATA NILIYOLIPIWA NA YESU INGAWA SIYAONI


Imani ni hati miliki ya vitu vyako ambavyo Mungu amekupa; lakini huvioni, huvisikii, huvigusi, huvinusi, hujaviona.


Ni hati milimi kwa njia ya Neno la Mungu. Inamiliki kwa njia ya Neno kutoka kwa Mungu: Kisha kuwaza imekuwa; kusema imekuwa na kutenda imekuwa.


Imani ni kuona mavuno tayari yametokea wakati mbegu ipo shambani: Hiyo kuandaa ghala, soko la kuuza na nyumba utakayojenga, baada ya mavuno.


Imani inasema, inashukuru, inashangilia na kumsifu Mungu kwa yale yote msalaba uliyotupa, kabla hayajadhihirika, lakini tayari yapo.


Imani ni kutotegemea ulimwengu wa macho, masikio au hisia. Ni kumiliki yasiyoonekana kwa Neno la Mungu tu.


1. Msalabani Alifanyika Dhambi upate Haki
*Unaona huna dhambi kwa imani yako kwa Yesu, maana amelipia dhambi msalabani: Akafufuka siku ya tatu uwe na haki (1Wakorintho 5:21, Warumi 4:25).


2.Msalabani Alifanyika Maskini Uwe tajiri
*Ingawa hauoni kwa macho una nyumba au chochote unachohitaji. Msalabani Yesu alikosa vyote ili wewe upate vyote. Alifanyika laana ya torati ya umaskini ili wewe upate utajiri wa Ibrahim. Unawaza hivyo na kusema hivyo maana tayari una hati miliki ya kutajirishwa, ingawa katika hali halisi haionekani hivyo (2 Wakorintho 8:9, Wagalatia 3:13).


3. Msalabani Alipigwa na kuumizwa wewe upone
*Ingawa unajisikia unaumwa tayari umemilikishwa uponyaji, maana umelipiwa na maumivu ya Yesu msalabani na kupigwa kwake. Yesu amefanyika, laana ya torati yaani magonjwa ili baraka ya Ibrahimu iwe juu yako yaani uponyaji (Mathayo 5:21, 2Petro 2:24, Wagalatia 3:21).


4.Msalabani Yesu amewanyang'anya mashetani silaha zote na kuwafanya si kitu, hivyo kukupa mamlaka juu yao.
*Amezivua enzi na mamlaka yaani nguvu za giza: Amezifanya si kitu msalabani, amezipoozesha msalabani, amezinyang'anya silaha msalabani, amezifanya sifuri msalabani. Nguvu za pepo wa magonjwa, tamaa, umaskini, uchawi na nyingine, tayari tunayo hati miliki ya kuzishinda kwa msasaba. Hii ni imani(Wakolosai 2:15, Luka 10:29).


5.Msalabani Alionewa , Alikataliwa, Alidharauliwa
*Alionewa nisionewe, Alidharauliwa niheshimiwe, Alikataliwa nikubalike. Tayari ninayo haya sasa yameshalipiwa (Isaya 53:3, Mathayo 27:46).


6.Msalabani hakuwa na Amani alikuwa na mahangaiko *Ili mimi niwe na amani
*Niwe na utulivu katika fikra na kukaa na uungu, kama vile sauti ya Mungu. Nisiogope chochote wala kujisumbua. (Isaya 53:5, 2Thesalonike 3:16, Warumi 15:33, Warumi 15:13).
KWA NJIA YA KIFO NA KUFUFUKA YESU NINAVYO VYOTE NINAVYOHITAJI PASIPO KUVIHISI AU KUVIONA. VINADHIHIRIKA KWA KUAMINI.

No comments:

Post a Comment