Monday, August 8, 2016

JINA LA YESU-2

WAFILIPI 3:10-11
Yesu yupo juu ya kila kitu, duniani, mbinguni na kuzimu. Hakuna aliye mkuu au kilicho kikuu kuliko Yesu. Ili kuweza kudhihirika duniani kwa nguvu na ukuu wake, jina lake linahitajika. Sio jina tu, Bali imani katika jina lake. Hii inajengeka tunapozidi kumjua na kumjua. Kwa nini tunaomba wakati wote? Kwa nini tunasoma Neno wakati wote? Kwa nini tunatafakari?;Ni Ili tuzidi kumjua. Tunapozidi kumjua, imani katika Yeye inakuwa dhahiri, matokeo yake jina lake linakuwa na matokeo makubwa zaidi tunapolitumia. Usiseme Yesu tu! Unaposema, nyuma yake umjue yukoje, ndipo jina hili litadhihirisha ukuu na uwezo wake.

No comments:

Post a Comment