Thursday, May 5, 2016

ALIKUWA SISI, TUWE YEYE

Yesu ni sadaka ya ukombozi alitolewa atukomboe au atununue toka katika kila uharibifu ambao ulitokea kwasababu ya dhambi. Alitolewa ayafidie maisha yetu yote (Marko 10:45).


Alitolewa ayachukue maisha yetu na hali zetu, ili atupe maisha yake na hali yake. Kuna vitu Yesu alipitia ili sisi tusipitie, kwa kusema hivi alitulipia. Kukombolewa ni kulipiwa na hatimaye kununuliwa.


Yesu alifanyika dhambi zetu, ili sisi tupate haki yake (2Wakorintho 5:21), Yesu alipigwa akaumwa mwili wake, sisi tusiumwe(Isaya 53:4). Yesu alikataliwa ili sisi tukubalike(Isaya 53:3), Yesu alifanyika maskini, sisi tuwe matajiri (2Wakorintho 8:9).Yesu aliadhibiwa ili sisi tuwe na amani (Isaya 53:5).


Yakatae maisha yako, usiyaangalie kisha yakubali maisha ya Yesu. Shetani anachopenda ni kukuonyesha maisha yako, Ikiwa ni mema au mabaya, anataka uyashike na kuyatazama hayo. Ukifanya hivyo utashindwa.


 Usijifikirie wewe katika kuweza kwako au kushindwa kwako, mtazame na kumfikiria Yesu.
Yakupasa kumfikiria Yesu, badala ya kujifikiria wewe.


Usijitazame wewe tu, mtazame Yesu aliyekuwa wewe,ili wewe uwe yeye. Fikiri alivyo mkono wa kuume, Biblia inaposema tuyatafakari na kuyafikiria yaliyo juu (Wakolosai 3:1-3), ina maanisha tumfikirie Yesu. Tusiyafikiriye tuliyonayo hapa duniani, tumfikiri Yesu na kumsema yeye.  Hii ni moja ya siri kubwa za kushinda dunia na majaribu ya aina zote.


SEMA: YESU ALIKUWA MIMI NILIVYO DUNIANI, ILI 'NIWE YEYE' ALIVYO MKONO WA KUUME.

No comments:

Post a Comment