Tuesday, April 26, 2016

Kuangusha Kisha Kuponda

KUANGUSHA KWA NGUVU NA KUPONDA KWA JINA


Katika Zaburi 44:5, maandiko yanasema kwa nguvu za Mungu tutawaangusha watesi wetu, kwa jina lake tutawakanyaga watupingao.
Kwa lugha ya sasa katika Agano jipya tunaweza kusema ; kwa Neno la Mungu tumewaangusha watesi wetu (maana Neno lina nguvu- Waebeania 4:12). Kuangusha hapa ni kama vile ng'ombe dume mkubwa mwenye nguvu asukumapo kitu na kuangusha. Kwa Neno la Mungu kinywani mwetu tunasukuma ushetani na kuuangusha kwa nguvu.


 Kwa jina la Yesu tunawakanyaga watupingao. Yesu alisema ametupa amri ya kuponda (kukanyaga), nyoka na nge na nguvu zote za yule mwovu (Luka 10:19). Kumbe! Ni kwa jina Lake tunakanyaga au tunaponda kazi za shetani.


MKAKATI WA KIVITA, ANGUSHA KWA NGUVU ZA NENO UTENDAJI WA SHETANI NA KUUPONDA BAADA YA KUUANGUSHA KWA JINA LA YESU. ANGUSHA KWA KUKIRI MAANDIKO, KISHA HARIBU AU PONDA KWA KUTUMIA JINA LA YESU.

No comments:

Post a Comment