Mungu analitazama Neno lake alitimize (Yeremia 1:12). Tafsiri ya ndani ya kulitazama Neno hapa ni: Kuliangalia tokea mwanzo mpaka mwisho litaakapotimia, kulilinda mpaka litakapotimia, kulifuata nyuma wakati linasemwa. Unapoliweka moyoni Neno la Mungu kumbuka Mungu analilinda mpaka litakapotimia. Unapolitamka analifuata nyuma katika kinywa chako alitimize.
Wakati wote usiache kushirikiana na Neno kwa kulisoma, kuliwaza, kulitenda; mtakuwa pamoja na Mungu wakati wote, alitazamapo Neno lake kwako atakuwa anakutazama wewe.
No comments:
Post a Comment