IV
ISHARA
YA KUNENA KWA LUGHA
Kunena
kwa lugha siyo Roho Mtakatifu, ni ishara ya kwanza ya nje inayodhihirisha mtu
amempokea Roho Mtakatifu ndani.
Roho
anaweza kumjaa mtu bila kunena kwa lugha! Ila ishara ya nje inayoonyesha amejaa
ni kunena kwa lugha. Watu wengi hujazwa Roho ila ishara ya kunena huwa
haijaonekana hii haina maana hawajajazwa bali ishara haijaonekana. Kuna
maandiko kadhaa yanaoonyesha kujazwa Roho au kumpokea Roho kunanendana na
ishara ya kunena kwa lugha:
Matendo
2:1-4 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste
walikuwako wote mahali pamoja. (2) Kukaja
ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza
nyumba yote waliyokuwa wameketi (3) Kukawatokea
ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. (4)
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. ”
Matendo 19:6 “Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu
yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”
Matendo 10:44-46, “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho
Mtakatifu akawashuki wote waliolisikia lile neno. (45) Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja
pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
(46) Kwa maana waliwasikia wakisema kwa
lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, (47) Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa
wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?”
Andiko lililopita
linaonyesha Waliotahiriwa walifahamu watu wamejazwa Roho maana waliwasikia
wakinena kwa lugha. Kulikuwa na
kiashirio kwamba wamepokea Roho na cho ni kunena kwa lugha.
Kitabu hiki kidogo
kimekuja ili kukusaidia kuweza kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha.
Kimekuja ili usikie kuhusu kumpokea Roho upate imani na baadaye ujazwe Roho na kunena kwa lugha. Nitataja mambo kadhaa hapa ambayo usiyasahau
ikiwa unataka kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha.
I.
Yesu Ameomba Roho
Mtakatifu kwa Baba kwa ajili yako (Yohana 14:16)
II.
Yesu Amempokea Roho
Mtakatifu toka kwa Baba kwa ajili yako (Matendo 2:33)
III.
Yesu Amekupa Roho
Mtakatifu toka kwa Baba (Matendo 2:33)
IV.
Mpokee Roho
Mtakatifu kwa imani, uliyosikia (Wagalatia 3:2)
Ikiwa unataka kujazwa Roho
mambo haya manne yasitoke ndani yako yatafakari na kuyasema, tumia maandiko
tuliyoyataja hapo nyuma.
V
MPOKEE ROHO MTAKATIFU
Katika kipengele hiki cha
mwisho, Mungu anakwenda kukusaidia kumpokea Roho na kuanza kunena kwa lugha.
Mara nyingi nimeona watu wakimpokea Roho na kunena kwa lugha wakiwa katika hali
ya imani ya kuyafanya haya. Ingawa siyo sheria kwamba, kwa hatua hizi ndiyo
utajazwa Roho.
I. Mwamini Yesu.
Mwamini
Yesu kwa kuoshwa kwa damu yake. Wakati wa maombezi au maombi binafsi ya ujazo
wa Roho, lazima kumwamini Yesu na kuzaliwa mara ya pili, kuwa na kisima. Hata
kama umeokoka ni vema kukiri wokovu na imani yako kwa Yesu ili kuweza kumpokea
Roho wake. Anasema, Aniaminiye mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake
(Yohana 7:37-39). Kumwamini Yesu ni msingi wa kumpata Roho (Mito). Roho anafanya
kazi na damu. Kipengele hiki ni cha kuhusisha damu ioshayo kabla ya Roho
Mtakatifu.
II. Ona Kiu
Yesu
alisema mtu akisikia kiu aende kwake anywe (Yohana 7:37). Roho Mtakatifu
unampokea kwa shauku kuu! Yaana kiu. Nakumbuka miaka ya themanini alikuja mhubiri
kutoka Kenya aitwaye George Gichana. Alikuwa akihubiri viwanja vya Jangwani Dar
es Salaam. Alipohubiri alikuwa akinena kwa lugha sana! Mimi nilitamani sana
nijazwe na ninene kwa lugha kama yeye. Siku moja baaada ya mkutano
nilijisemesha moyoni “leo ni leo lazima ninene kwa lugha”. Nilitoka katika
mkutano nikiwa na hamu kuu ya kujazwa Roho na kunena kwa lugha. Nilipofika
nyumbani, moja kwa moja nilienda kibalazani, nikapiga magoti na kwa shauku kuu
nilianza kusema, “Haleluya, haleluya, haleluya,…” Ghafla nikaanza kunena kwa
lugha!
Yesu
alisema anayeona kiu aende kwake anywe maji ya Roho, ni kweli niliona kiu
nikaenda kwa Yesu akaninywesha maji ya Roho. Hapa udhihirisho wa karama za Roho
pia unaendana na kuzitamani, kuona kiu.
III. Simama Mbele za Yesu
Unapotaka kumpokea Roho
usitazame mtu, ikiwa ni mhubiri au mchungaji ! Yesu ndiye anayebatiza kwa Roho.
Toa macho yako kwa watu wanaoomba au kukuombea, mtazame Yesu kwa imani kwamba
yupo mbele yako anakujaza Roho. Luka 3:16 imeandikwa, “Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini
yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya
viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”. Simama mbele
za Yesu huku umefumba macho kwa imani na kusema, “Yesu unanijaza Roho
unanibatiza kwa Roho kama maandiko yasemavyo, katika jina la Yesu lolote
nilisemalo katika jina lako unalifanya. Yohana 14:14. Hatua hii ya imani ni nyeti kabla ya
udhihirisho kutokea. Endelea kusema na kung’ang’ana. Sema “Yesu ni wewe
unamjaza Roho”.
IV. Hisia za Kiroho
Wakati wa kujazwa unaweza
kuanza kujisikia furaha, au kulia au hofu ya Mungu. Mara nyingine unaweza
kuanza kujisikia mwepesi. Unajua ujazo wa Roho mara nyingine unaendana na hisia
au matukio. Mfano matendo ya mitume 2, kulitokea uvumi wa upepo, ndimi za moto,
kabla ya kuanza kunena! Wakati unaongea na Yesu unaweza kuanza kupata hisia na
mabadiliko.
V. Tendo la Imani
Chukua
hatua ya imani ya kusema na kuacha mdomo wazi. Maandiko yanasema, “Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha
toka nchi ya Misri; Fumbua kinywa chako nami nitakijaza” (Zaburi 81:10).
Unaposema mbele za Yesu mfano “Yesu unanijaza, Yesu ni mwema …..” Sema huku
unaachia sekunde chache mdomo wako ukiwa wazi. Ufanyapo hivi na kusikia unataka
kulia, kufurahi nk, basi ni dalili tayari Roho yupo na wakati wowote
utanena kwa lugha!
VI. Chemchemi Zatoka Ndani
Maandiko yanaposema
amwaminiye Yesu, Ndani yake zitatoka
chemchemi (Roho). Katika maandiko maana halisi isemayo ndani yake ni
ndani ya `tumbo la kiroho’. Roho anatokea ndani, anajaa tokea ndani na
anadhihirika nje kwa kunena kwa lugha.
Zipitie hatua hizi ukiwa
peke yako utashangaa, utanena kwa lugha, wengi wamenena kwa kujifunza somo hili
na kulifanyia kazi.
Baada ya kujazwa Roho na
kunena kwa lugha, endelea kunena kwa lugha na kujijenga kwa kunena kwa
lugha. Soma kitabu kiitwacho Kushirikiana
na Roho Mtakatifu, ili kuzidi kumwelewa Roho.
Karibu!
No comments:
Post a Comment