II
KABLA
YA KUJA ROHO MTAKATIFU
Labda, turudi nyuma kidogo
tuangalie kwa kifupi kabla ya kuja Roho Mtakatifu duniani mambo gani ilikuwa
lazima yatangulie.
1.
Kuja kwa Yesu
Kabla
ya Roho Mtakatifu kuja, ilikuwa ni lazima Yesu aje kwanza, ni kama ilivyokuwa
kwa Yohana Mbatizaji, kabla ya kuja Yesu ilikuwa lazima aje Yohana mbatizaji, Maandiko
yanasema, “Hata siku ya mwisho, siku ile
kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,
na aje kwangu anywe. (38) Aniaminiye
mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani
yake (39) neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio
watampokea baadaye; kwa maana roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.” (Yohana
7:38-39). Andiko hili linaonyesha ni mpaka Yesu aje, Afe, Afufuke, na atukuzwe
ndipo Roho anatokea.
2.
Kuondoka kwa Yesu
Yesu
alisema, “Lakini mimi nawaambia iliyo
kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi
hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.“ (Yohana 16:7)
Kuondoka kwa Yesu duniani ni kuja kwa Roho Mtakatifu duniani. Huu ni uhakika wa
kumpokea. Unaweza kumpokea Roho kwa kuwa Yesu ameshaondoka!
3.
Kuomba kwa Yesu
Yesu
anasikiwa na Mungu siku zote! Alisema “……
Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. (42) Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya
mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma” (Yohana
11:41-42). Kati ya maombi ya Yesu ambayo yameshajibiwa kwetu na Baba aliyoomba Yesu
yanaonekana katika maandiko haya “Nami
nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele”
(Yohana 14:16). Yesu anasema, naye atamwomba Baba na Baba atatupa Msaidizi
mwingine yaani Roho Mtakatifu. Inaonekana katika maandiko haya ni kitu
kirahisi! Alitupa lini? Au maombi hayo yalijibiwa lini? Yalijibiwa Roho
aliposhuka wakati wa Pentekoste, Matendo 2:1-3. Sasa imebaki wewe kupokea tu,
Yesu ameshajibiwa maombi yake, aliomba Roho akapewa sasa unampokea! Kirahisi
bila kuhangaika.
4.
Kuketi kwa Yesu
Yesu
alipoomba kwa Baba tupewe Roho Mtakatifu Baba alijibu. Alimpa Yesu Roho
Mtakatifu na Yesu akatupa sisi. Inaonekana Baba alimpa Yesu Roho kwa ajili yetu
baada ya Yesu kufufuka na kuketi mkono wa kuume wa Mungu.
Yesu
aliposema atamwomba Baba Msaidizi mwingine inawezekana kabisa alikuwa na maana
ya kumwomba akiwa mkono wa kuume wa Mungu maana maandiko yanaonyesha hapo ndipo
alipompokelea na kutupa sisi, “Basi yeye,
akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi
ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia“
(Matendo 2:33).
Mpaka
hapa fahamu ya kuwa Yesu amemwomba Baba Roho Mtakatifu. Baba akampa mkono wa
kuume na yeye Yesu akatupa sisi. Wajibu wetu sasa ni kumpokea! Siyo
kumbembeleza Mungu atupe! .
III
SURA
ZA ROHO NDANI YA MWAMINI
Roho
Mtakatifu kwa mwamini anaonekana kwa sura mbili. Sura ya kwana ni `Chemichemi’ na sura ya pili ni ‘Mito’.
JUMAPILI
YA KUFUFUKA (Chemchemi)
Biblia
inasema “Yesu akajibu, akawaambia, Kila
anywaye maji haya ataona kiu tena; (14) Walakini ye yote atakayekunywa maji
yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa
ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.” (Yohana
4:13-14). Chemchemi inayotajwa hapa tafsiri yake rahisi ni kisima. Kisima ni
cha mtu au watu fulani. Kisima kinaweza kuwa na ubinafsi. Unaweza kukifunga au
kuruhusu watoto wako tu watumie nk. Roho Mtakatifu anaweza kuonekana kama
kisima ndani yetu, yeye ni mmoja atuwezeshaye kuwa na mahusianao ya moja kwa
moja na Mungu sisi kama watu binafsi mmoja mmoja. Yeye Roho Mtakatifu ndani
yetu ni chemchemi za maji zibubujikiazo uzima wa milele.
Ukisoma
maandiko Yohana 20:19-22, imeandikwa, “Ikawa
jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango
imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia,
Amani iwe kwenu. (20) Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na
ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana (21) Basi Yesu
akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami
nawapeleka ninyi. (22) Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia,
Pokeeni Roho Mtakatifu.”
Baada
ya Yesu kufufuka na kukutana na wanafunzi, Biblia inasema hapa, akawavuvia
akawaambia wapokee Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma,
Jumapili ya ufufuo. Kwa kuvuviwa Roho Mtakatifu wanafunzi walikuwa wakizaliwa
kwa Roho Mtakatifu. Kufufuka kwa Yesu ndiyo mlango wa watu kuzaliwa mara ya pili kwa Roho Mtakatifu. Yesu
alipowavuvuia Roho alikuwa anawazaa mara ya pili. Tayari walikuwa wanamwamini na
kumkiri Yesu kama Bwana kabla hajafa, Lakini walibadilishwa na kuzaliwa mara ya
pili baada ya Yesu kufufuka. Ili mtu
azaliwe mara ya pili ni lazima amkiri Yesu kama Bwana na aamini Mungu alimfufua
katika wafu, Wanafunzi tayari walikuwa wanamkiri Yesu kuwa ni Bwana ila bado
alikuwa hajafufuka, hivyo wasingeweza kuokoka/kuzaliwa mara ya pili kabla
hajafufuka, Hivyo baada ya kufufuka waliweza kuamini kuwa Mungu alimfufua
katika wafu, Wakavuviwa Roho Mtakatifu, hapa walikuwa wanaokoka wanazaliwa kwa
Roho, “Kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa
chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika
wafu, utaokoka” (Warumi 10:9).
Sehemu
hii ya kuvuviwa Roho, Roho Mtakatifu alikuwa ni kama KISIMA au CHEMCHEMI. Hatua
hii ni hatua ya mahusiano ya mtu binafsi na Mungu, kuzaliwa kwa njia ya Roho
Mtakatifu, “Yesu akajibu,
akamwambia,Amin, amin nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona
ufalme wa Mungu. (6) Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa
Roho ni roho ” (Yohana 3:3,6).
Tunaposema
kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu tunamaana hii, “Kila mtu aliyeokoka ana Roho kama Kisima amenyweshwa Roho Mtakatifu
anaye Roho wa Kristo.” Kuna watu husema kila mtu aliyeokoka ana Roho wa
Kristo, ni kweli kwa maana ya kila aliyeokoka amezaliwa na Roho wa Kristo na ni
mali ya Kristo,”Lakini ikiwa Roho wa
Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini
mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” (Warumi 8:9).
Mtu
huyu aliyezaliwa mara ya pili ni kweli ana Roho Mtakatifu, lakini ni kwa ngazi
ya kisima anachotumia yeye na watu wachache. Anatakiwa asasifi toka Jumapili ya
kufufuka Yesu yenye kisima/kuzaliwa na Roho, mpaka afike Jumapili ya Pentekoste,
yaani siku ya kwanza ya juma aliyoshuka Roho Mtakatifu na kuwajaa mitume.
JUMAPILI
YA PENTEKOSTE (Mito)
Jumapili
hii ni Jumapili ya MITO na sio KISIMA. Hata hivyo huwezi kuingia Jumapili hii
ya Pentekoste kabla ya Jumapili ya kufufuka. Ni lazima kuzaliwa kwa Roho kwanza
na kupata kisima kabla ya kujazwa Roho na kupata mito. Biblia inasema, “(37) Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya
sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje
kwangu anywe. (38) Aniaminiye mimi,
kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
(39) Na neno hilo alilisema katika habari
ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa
hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.” (Yohana 7:37-39). Maandiko
haya yalidhihirika wakati wa Pentekoste, “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste
walikuwako wote mahali pamoja.
(2) Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi
kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa
wameketi (3) Kukawatokea ndimi
zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. (4) Wote wakajazwa
Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia
kutamka. ” (Matendo
2:1-4).
Mto
una nguvu kuliko kisima. Mto hauna ubinafsi, hamna mtu anayeweza kuufungia mto
kama tufanyavyo kwa visima. Mto Nile ni wa Uganda, Sudani, Misri nk. Wote hawa
wana haki nao. Ndivyo ulivyo ujazo wa Roho Mtakatifu, unaathiri eneo kubwa
zaidi ya kuokoka na kuzaliwa mara ya pili. Unakuathiri wewe, jinari zako na
dunia kwa ujumla. Aliyejazwa Roho anaweza kufika Marekani akiombea mtu kwa
lugha akiwa Tanzania! Hamna mipaka.
Tunajazwa
Roho Mtakatifu ili tufikie mbali katika Yesu Kristo. Tuwe na karama,
tumdhihirishe Yesu kuwa yu hai amefufuka, Tuidhihirishe kazi yote ya msalaba
kwa Roho Mtakatifu.
Kumpokea
Roho Mtakatifu ni kujazwa Roho Mtakatifu. Tunaposema kumpokea Roho katika
kitabu hiki hatuna maana ya kuvuviwa Roho, yaani kuzaliwa kwa Roho na kuwa ‘kisima’.
Tunamaana ya kuzamishwa ndani ya Roho na kuwa na `Mito’.
Katika
Kanisa la kwanza ilikuwa ni kawaida kumpokea Roho Mtakatifu, baada ya kumwamini
Yesu. Ilikuwa ni kawaida kupokea mito baada ya kisima, “… akawauliza, Je! Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La,
hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu “ (Matendo 19:2).
Andiko
hili linatuonyesha vitu kadhaa. Kwanza baada
ya kuamini iliwapasa wampokee Roho. Pili iliwapasa wasikie kuhusu Roho ili wampokee. Kwa nini wasikie? Ni
ili wawe na imani ya kumpokea, Maana imani huja kwa kusikia, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na
kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Sababu moja kuu ya watu
kutompokea Roho Mtakatifu ni kutosikia kuhusu Roho, hatimaye kutokuwa na imani
ya kumpokea Roho. Roho anapokelewa kwa imani, “Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya
sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? ” (Wagalatia 3:2)
No comments:
Post a Comment