Wednesday, August 26, 2015
Vinavyoonekana Vinabadilika kwa Visivyoonekana
LEO ASUBUHI. MOYO WANGU UMENIKUMBUSHA KWAMBA VINAVYOONEKANA NI VYA MUDA TU. KUNA JAMBO NILIKUWA NIKILITAZAMA NA KULIFIKIRIA NAONA HALIWEZEKANI. NDIPO WAKATI NAENDESHA GARI GHAFLA! NIKAKUMBUSHWA KWAMBA, CHOCHOTE KINACHO ONEKANA KINAWEZA KUBADILIKA. ILA NENO HALIBADILIKI NA LINABADILISHA INGAWA HALIONEKANI.
MAANDIKO YANASEMA,
Majani yakauka,ua laanguka, Bali neno la Mungu litasimama milele ( Isaya 40:8).
Na kama mavazi utazizinga nazo zitabadilika lakini wewe ni wewe yule na miaka yako haitakoma (Waebrania 1:12).
Tusiviangalie vinavyoonekana, Bali visivyoonekana. Kwamaana vinavyoonekana ni vya muda tu; Bali visivyoonekana ni vya milele (2 Wakorintho 4:18).
HALELUYA! YUPO MUNGU ASIYEONEKANA, NA NENO LISILOONEKANA, HAWA WAWILI WANADUMU MILELE HAWABADILIKI. NCHI NA MBINGU ZITAZINGWA NA YEYE NA KUBADILIKA, MAJANI YANAKAUKA NA KUPOTEA YANABADILIKA. KINGINE CHOCHOTE TOFAUTI NA MUNGU NA NENO LAKE KINAWEZA KUBADILIKA. UGONJWA UNAOUSIKIA MWILINI NI WA MUDA TU, UNABADILIKA NA UPONYAJI WA NENO LISILOBADILIKA UNATOKEA. KUTOWEZA KUTENDA JAMBO FULANI UNAKOKUONA NI KWA MUDA TU, NENO LILILO NGUVU ZA MUNGU LISILOONEKANA NI LA MILELE LINABADILISHA HALI HIYO!
Siku zote kumbuka vitu unavyoviona ni vya muda tu, na vinabadilishwa na vitu visivyobadilika vya milele, yaani Mungu na Neno lake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hakika tunapaswa kuvingangania vile visivyoonekana zaidi.Kwani visivyoonekana huleta udhihirisho kwa vinavyoonekana.Mfano mzuri ni upepo huwa hatuuoni ila matokeo yake huwa yanaonekana, umeme huwa tunaona matokeo tuu ila wenyewe hatuuoni.Hali kadhalika Neno/Mungu/Roho Mtakatifu akiwepo mahali tutaona matokeo yake tu!
ReplyDeleteBarikiwa mtumishi wa Mungu aliye hai kwa neno zuri la asubuhi ya leo!