Imani ya Kumsikia Mungu
“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu,
awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani,
pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka
ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku
na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.” (Yakobo 1:5-7).
Inakupasa kuijenga imani yako katika eneo la kumsikia Mungu. Kila kitu
tunakipata kwa neema kwa njia ya imani toka kwa Mungu. Ikiwa ni uponyaji
twaupata kwa imani, ikiwa ni majibu ya maiombi twayapata kwa imani nk. Si hayo
tu, hata sauti ya Mungu twaweza kuisikia kwa kujenga imani zetu eneo la
kumsikia. Somo hili fupi litakusaidia kuweza kumsikia Mungu.
Ujengapo imani yako ndani ya maandiko yafuatayo utaweza anza msikia
Mungu
1. Maandiko yanasema imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la
Kristo (Warumi 10:17).
Kumsikia Mungu huja kwa Neno la
Kristo. Bila Neno ndani yako usitegemee kumsikia Mungu. Mungu husema akiwa
ndani ya Neno. Usomapo, usikiapo, usemapo maandiko, Mungu huwa nyuma yake
tayari kusema. Akisema kwa namna hii imani hutokea. TAFUTA SANA KUMSIKIA MUNGU
KWA KUTAFUTA SANA KUYAELEWA MAANDIKO. KATIKA HAYO UTAISIKIA SAUTI YAKE.
2. Maandiko yanasema wakati wa sasa Mungu anasema nasi katika Mwana
(Waebrania 1:1-2)
Kumsikia Mungu huja kwa njia ya
Yesu Kristo. Usitafute kumsikia Mungu nje ya Yesu Kristo. Yeye ni Sauti ya
Mungu kwetu, katika yeye Mungu husema nasi. Sauti yeyote katika ulimwengu wa
roho lazima ipimwe na tabia ya Yesu, au Yesu alivyo. Kwa mfano ukisikia sauti
inakwambia “utakufa leo” na kuanza kusikia woga usiseme ni Mungu, maana Yesu,
husema usiogope na pia yeye ni uzima.
3. Maandiko yanasema kondoo huijua sauti ya mchungaji na kuisikia (Yohana
10:4, 27)
Ikiwa umempa Yesu maisha yako
wewe ni kondoo wa Mungu, tayari unao uwezo wa kumsikia Mungu. Maandiko haya
yanaonyesha unaweza kumsikia kana kwamba tayari unamsikia! Anza kuwaza na
kusema hivyo imani yako ya kumsikia Mungu inaonezeka. Hutafuti kumsikia Mungu
tayari unako, inakupasa tu kujenga mazingira ya kumsikia.
4.Mungu husema ndani ya roho zetu kwa Roho wake (Warumi 8:16)
Roho iliyozaliwa mara ya pili
inaweza kuongozwa na Mungu kwa ufahamu wa rohoni. Sauti ya Mungu ya kawaida
huja kwa hali ya ufahamu wa rohoni nam ushuhuda wa Roho ndani. Hii sio sauti
kubwa ya kusikika na masikio, bali ni sauti ya kufahamu na kuelewa kwa ndani.
Unaweza ukawa unaelewa kitu moja kwa moja na kwa mtiririko! Bila kusikia sauti
kubwa. Hii ni sauti ya roho yako katika Roho Mtakatifu. Hujengeka sana katika
kunena kwa lugha na kutafakari Neno.
MUHIMU: Mungu anasema nasi kwa namna nyingine nyingi. Ila hizi
chache ni nzuri kuanza nazo maana zina usalama wa kiroho zaidi. Wakati mwingine
tutajifunza jinsi ya kupima sauti ya Mungu. Penda kumsikia kwa ufahamu wa Neno
na Roho katika roho yako, zaidi ya kusikia kupitia watu au malaika au ndoto.
Mungu hutumia hivi pia, ila usivitafute sana, kaa na Neno kwanza.
Kwa Nini Anasema Nasi?
1. Ili kutufundisha 2. Kutuongoza
3. Kutuonya 4.Kutulisha 5.Kutufariji 6.Kututia nguvu 7.Kutupa silaha za vita.
Namna ya Kumsikia
1. Husema tutakapo kusikia
2.Husema tusemapo naye
3.Husema tukaapo na maandiko yake
kwa wingi
4.Husema tukiwa na furaha na
kuimba
5.Husema katika mioyo miyepesi
iliyosamehe
6. Husema tumkaribiapo kwa
kufunga
7.Husema tutendapo asemayo
No comments:
Post a Comment