TUTATOA HESABU
Kutoa hesabu ni kurejesha taarifa kwa aliyekutuma au aliyekupa mamlaka ya kutenda mambo fulani. Nakumbuka Wanajeshi wa Tanzania, baada ya vita vya Kagera waliporudi, walisema, "Kazi Mliotutuma tumemaliza" Kwa usemi huu walikuwa wakitoa hesabu.
Maana moja wapo ya wakili ni mtetezi. Maana nyingine ya wakili, ambayo hatuitumii sana ni mtoa hesabu. Ukipewa kipawa au jukumu lolote tayari wewe ni wakili, ni mtoa hesabu. Kupewa maisha kama binadamu tayari tunakuwa watoa hesabu, wa maisha yetu mbele za Mungu, tuliyatumiaje mbele za Mungu kwaajili ya YESU. Tunapookoka tayari ni watoa hesabu, tunautumiaje wokovu na vipawa vya wokovu.
Kila binadamu ni wakili, ni mtoa hesabu kwa Mungu. Katika wito, tutatoa hesabu, tulifanya nini na zawadi tulipewa ya Yesu Kristo; 1. Tulimwamini? Tulimtukuza?Tulimfuata? Tulimtanguliza? Tulimtangaza? Tulimwonyesha kwa wengine?Pamoja na yote ufanyayo hapa duniani, kumbuka siku moja utatoa hesabu mbele za Mungu kama wakili, maisha, vipawa na kipawa kikuu "Yesu Kristo".
Tutatoa hesabu, tilitumiaje muda wetu tuliopewa kwaajili ya Yesu. Kama ulipewa karama fulani, utatoa hesabu uliitumiaje. Ulitumia kwaajili ya Kristo, au kwaajili yako. Unaposema una upako, upako ni mzuri, lakini hatari yake ni utatoleaje hesabu upako huo? Uliutumia kujisifu au kwa kumsifu Yesu.
Kutomsifu Yesu baada ya kutumika kwa upako wa Roho wake ni wizi wa utukufu wake. Imemgarimu Mungu kifo cha Yesu upako huo kuonekana! Hivyo sio kitu cha kuchezea! Ili kutafuta sifa na utukufu wetu.
Utoa hesabu kwa maneno yako unayoongea, mwili wako unavyooutumia, Fursa zako, mfano eneo unalofanya kazi nk. Maisha yetu yote yana uwakili ndani yake na kutoa hesabu. Kila ufanyapo kitu, kumbuka utatoa hesabu, hakiishii hapo tu!
Usiache kusoma maandiko haya: MATHAYO 12:26, MATHAYO 18:20-25, LUKA 16:1-3, WARUMI 14:12, 2 WAKORINTHO 5:20, 1WAKORINTHO 4:1-2, 1PETRO 4:5.
JIANDAE KUTOA HESABU NZURI KWA MUNGU. HAKIKISHA KILA UFANYACHO MSINGI WAKE NI YESU. HESABU ZAKO ZITAKUWA NA MANUFAA KATIKA YESU. USIJENGE MAISHA, HUDUMA, NA CHOCHOTE KILE BILA YESU KRISTO.
No comments:
Post a Comment