Wednesday, July 29, 2015

Utendaji wa Damu

1. Kazi za damu mwilini
Kusambaza chakula
Kusambaza hewa
Kutoa sumu katika mwili
Kulinda na magonjwa
Ni uhai wa mwili

2. Kazi za damu kiroho
Inaishika roho katika mwili, damu ikitoka roho haiwezi kukaa katika mwili. Yesu alipomwaga damu roho yake ilitoka mwilini.
Damu inabeba 'sauti' ya roho ya mwenye nayo (Waebrania 12:24).
Damu inaunganisha ulimwengu unaoonekana na usioonekana. Kuna vitu viwili vikubwa viwezavyo kuunganisha ulimwengu unaoonekana na usioonekana: Damu na maneno.

Mahali pa muunganiko huo panaitwa madhabahu. Ikiwa ni chini ya mti au popote, damu inapomwagwa na maneno kusemwa, roho huachiliwa, hapo ni madhabahu.

1. Madhahuni panafanyika makubaliano kwa njia ya maneno kati ya mtu na miungu au Mungu asiyeonekana. Makubaliano haha huitwa 'agano'.
2.Maneno ya madhahu husemwa kwa njia ya damu, haya yanaachilia nguvu toka ulimwengu usioonekana kuja ulimwengu unaoonekana.

               MSALABA NI MADHABAHU
UJUMBE HUU NIMEHUBIRI JUMAMOSI ILIYOPITA KATIKA MKUTANO WA NJE, DUMBETA.
                         Walawi 17:11-12
                          1Petro 1:19-20
                          1Yohana 5:7-9
                         

No comments:

Post a Comment