ANATAFUTA NAFASI KWA KUSUMBUA NA KUUDHI
Kusumbuana kuudhi kwa nje, huku ni kusonga hasa kwa maneno, mpaka mtu anaufungua moyo, Soma Waamuzi 16:16.
Delila alimsonga Samsoni na kumsumbua kwa maneno mpaka akafungua moyo:
1.Akalegeza msimamo
2.Akafungua moyo wake
3.Akachoka kustahimili
Kusumbua na kuudhi kwa nje ni mbinu ya kishetani kukufanya ulegeze msimamo Wako kiungu. Mbinu hii huitumia kwa kutumia mtu wa karibu na wewe. Kila siku anaweza kutenda mambo fulani au kusema, mpaka uchoke, kama ni katika ndoa mpaka useme 'naondoka', kama ni huduma useme 'naacha'. Anaweza kuwa mtoto, mzazi, Baba, Mama au mwingine.
JAMBO LA KUFANYA
Soma Waebrania 12:1-3, Silaha ya kutobadilisha msimamo Ni kumtazama Yesu, kumsema Yesu. YEYE NI MWAMBA, mwamba ni msimamo.
YEYE NI SILAHA YA MKANDA WA KWELI, mkanda WA kweli ni msimamo.
Mseme Yesu, muimbe Yesu, mfikirie Yesu, katika yeye msimamo Wako hautayumba.
USIBADILISHE MSIMAMO WAKO
KATIKA KUMPENDA MUNGU.
No comments:
Post a Comment