Monday, July 20, 2015

Nguvu ya Mungu

Nguvu ya Mungu kati yetu ni Yesu
Yeye ni:

1.Nguvu ya kuumba
2.Nguvu ya kurejesha
3.Nguvu ya kumilikisha
4.Nguvu ya kuhuisha
5.Nguvu ya kutiisha

ALITOLEWA KATIKA UDHAIFU KAMA MWANAKONDOO, ANAISHI KWA  KWA NGUVU YA MUNGU KAMA KUHANI KATI YETU.

Kwa Neno lake Kristo anafunuliwa kati yetu kama mwenye nguvu. Katika Agano la kale nguvu ya Mungu, ilitegemeana na alichofanya mtu kwa kuitii sheria. Hapo ndipo Mungu alifanya jambo. Hata hivyo Wayahudi hawakuweza kuitii sheria, Mungu akawapa huduma ya upataisho: Sadaka za wanyama na Makuhani, ili aendelee kukaa nao bila kuwaangamiza.

Agano jipya nguvu ya Mungu ipo katika Yesu Kristo kwa ulimwengu mzima! Kwa kila aaminiye na sio Wayahudi tu. Yeye ndio sadaka ya upatanisho na kuhani. Alitolewa katika udhaifu kama mwanakondoo, yaani sadaka. Sasa anaishi kwa nguvu za Mungu kama kuhani. Kwakuwa imani zetu zipo kwake sisi pia tunaishi kwa nguvu ya Mungu, kwa njia yake aliye ndani yetu.
             2 WAKORINTHO 13:4

No comments:

Post a Comment