. Kumbukumbu 11:8
"Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi muivukiayo kuimiliki"
Neno la Mungu ndio nguvu ya kutumilikisha yale yaliyo haki yetu katika Yesu Kristo. Wana wa Israeli waliagizwa katika andiko hilo hapo juu, wayaangalie maagizo ya Mungu, maana katika hayo watapata nguvu ya kuingia katika nchi ya ahadi.
Bila shaka hata sasa, maandiko na ahadi za Mungu ndio nguvu ya kutumilikisha urithi wetu ambao Yesu ameununua msalabani; Neema, Kushinda, Utakatifu, Uponyaji nk.
Tunaugusa uungu na kuushiriki kwa njia ya Neno Lake. Usiache kukutana na Neno mara kwa mara, utashiriki uungu na kupata neema ya kuudhihirisha urithi wako.
No comments:
Post a Comment