KIUNGO CHA MUHIMU
Moyo, Ubongo, figo ni sehemu za muhimu sana katika mwili, bila hizo, uhai wa mwili hauwezi tegemezwa. Ulimi pia ni sehemu ya muhimu zaidi, yenye kuweza kutegemeza maisha ya kimwili, Kama vile kutafuna chakula, na kiroho pia, Kama vile kukiri maandiko, kutubu nk. Ulimi ni kiungo cha muhimu zaidi, maana kinahusika na ulimwengu wa mwili na roho, pia maisha yako ya sasa na baadaye. Viungo vingine vinahusika na maisha ya kimwili tu, na ya sasa tu. Soma na kushika maandiko haya ili kuweza kudhibiti ulimi wako.
Mithali 13:3
Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; bali afunguaye midomo yake atapata uharibifu.
Mithali 21:23
Mtu azuiae kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu.
Mithali 15:4
Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.
Mithali 18:7
Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
Mithali 18:21
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
Mithali 10:19
Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiae midomo yake hufanya akili.
Zaburi 34:11-14
Njoni, enyi wana,mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana.
Ni nani mtu yule apendezwae na uzima, apendaye siku nyingi apate kuona mema?
Uuzuie ulimi wako na mabaya, na midomo yake na kusema hila.
Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
Yakobo 3:1-2
Ndugu zangu msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa tutapata hukumu kubwa zaidi. Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu."
Yakobo 1:26
Mtu akidhani yakuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai." (Yakobo 1:26).
Mithali 18:8
Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
Walawi 19:16
Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana.
Yakobo 3:6
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Zaburi 109:3
Naam kwa maneno ya chuki wamenizunguka, wamepigana nami bure.
Yeremia 9:3-5
Huupinda ulimi wao, kama kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya mpaka ubaya. Wala hawanijui mimi asema Bwana. Jihadharini kila mtu na jirani yake; Wala msimtumaini ndugu awaye yote, maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huko na huko na kusingizia. Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoeza ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.
Mithali 20:17
Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu. Lakini halafu, kinywa chake kitajaa changarawe.
Mithali 12:6
Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.
Mithali 12:14
Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; na mwanadamu atarudishiwa matendo ya mikono yake.
Mithali 12:18
Kuna anenaye bila kufikiri,kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.
Mithali 18:4
Maneno ya kinywa cha mtu ni Kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; Chemchemi ya hekima.
Mithali 18:20
Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
Moyo, Ubongo, figo ni sehemu za muhimu sana katika mwili, bila hizo, uhai wa mwili hauwezi tegemezwa. Ulimi pia ni sehemu ya muhimu zaidi, yenye kuweza kutegemeza maisha ya kimwili, Kama vile kutafuna chakula, na kiroho pia, Kama vile kukiri maandiko, kutubu nk. Ulimi ni kiungo cha muhimu zaidi, maana kinahusika na ulimwengu wa mwili na roho, pia maisha yako ya sasa na baadaye. Viungo vingine vinahusika na maisha ya kimwili tu, na ya sasa tu. Soma na kushika maandiko haya ili kuweza kudhibiti ulimi wako.
No comments:
Post a Comment