Friday, June 12, 2015

Semina 1: Mch Wallace Howahowa

KUKUA KIROHO

Kukua kiroho ni kitendo cha kuongezeka kwa ufahamu wa rohoni na kuongezeka kwa uhusiano wa mtu binafsi na Roho Mtakatifu.

 Maombi ni chombo kimojawapo cha kuboresha uhusiano na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Ayubu 22:21-24, Utakusudia jambo nalo litatendeka. Pamoja na changamoto zote zinazo onekana hali ya nje haitakubadilisha ndani. Samaki wa maji chumvi hana chumvi ndani pamoja na kukaa katika chumvi. Pamoja na changamoto, bado Mungu atajipatia watakatifu.

Kukua katika kumjua Mungu ni muhimu, 2Petro 1:2; Neema iwe kwenu na amani. Neema na amani vinaongezeka tunapoendelea kumjua Mungu.

Neema ni nguvu ya uwezesho, itaongezeka katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. Unapokusudia kuendelea kumpendeza, Mungu anakuwezesha.

Katika kumjua Mungu kuna siri ya kubadilika. Usijenge tabia ya kusikia unayoyataka tu! Pia mtumikie Mungu kwa moyo wa kumkubali(1Nyakati 28:9-10).

Ukitaka kufaulu katika kumjua Mungu, Mtumikie kwa moyo mkamilifu-Jitoe kwake, Mungu anapendezwa na moyo huo.

 Kumkubali, maana yake kuna mambo mengine Mungu atafanya tofauti na ulivyofikiri. Hakuna kitu kibaya kama kutupwa na Mungu.

Ushuhuda wa kaka aliyeoa kilema. Mungu alimuongoza amwoe kilema, baadaye akamponya katika mkutano wa nje. Yule kaka alimtumikia kwa moyo wa kumkubali Mungu, kwa lolote!

 1Yohana 5:20, nasi twajua Mwana wa Mungu amekuja atupe akili. Akili njema ni ile ambayo inamtaka Mungu. Inampa Mungu nafasi ya kwanza. Akili hii amekuja kutupa ni akili ya kutusaidia kumjua.

KINACHOSABABISHA WENGI WASIKUE KATIKA KUMJUA MUNGU

 1. Utupu
Mtu yupo kanisani lakini ni mtupu (Mathayo 13:1-4, 18).
Moyo wake hajafaulu kuunyenyekeza apokee maneno ya Mungu. Ndege wanaotajwa hapa ni utendaji wa Ibilisi, unafunga ufahamu usiweze kupokea.

Kuna watu, Kila ukorofi ukitokea kanisani wamo. Ukiwa tupu huwezi kuchukua hatua za maendeleo ya kiroho. Upatu uvumao unaotajwa 1Wakorintho 13 ni kupiga kelele kama debe tupu.

2.Kukosa Kina, Math 13:5, 20
Wako watu wako kanisani wanachukua hatua baraka jambo likitokea. Hutakiwi kukimbia nyumba ya mapepo. Bundi akilia usiku anasifu, lakini wewe unakimbia!

3. Kuupenda Ulimwengu
Wanaoupenda ulimwengu, wanachanganya maisha yao na ulimwengu, shughuli za dunia na udanganyifu wa mali.

Mjue sana Mungu, ndipo mema yatakujia. Muombe Mungu pesa zikufuate. Usishikamane na ulivyopewa shikamana na anayetoa.

(HAYA NI BAADHI YA MANENO ALIYOSEMA MTUMISHI KATIKA SEMINA YA LEO).

No comments:

Post a Comment