UNAZO FUNGUO
I. Unaona nini katika Maandiko
haya kuhusu funguo
A. Ufunuo 1:17-18, “…Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nilikuwa
nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele, nami ninazo funguo za mauti
na za kuzimu”
B.Ufunuo 3:7, “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo
yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye,
naye afunga wala hapana afunguaye”.
C. Ufunuo 3:8, “Tazama,
nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa
kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina
langu.”
D. Ufunuo 20:1-3, “Kisha
nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu na mnyororo
mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, Ambaye ni
Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu.”
E. Isaya
22:22, “Na ufunguo wa nyumba ya Daudi
nitauweka bagani mwake, yeye atafungua
wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.”
1. FUNGUO NI UWEZO WA
KUFANYA JAMBO BILA MIPAKA
Yesu
alisema amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani(Mathayo 28:18:),
Tafsiri yake nyingine anao uwezo wa kutenda mbinguni na duniani. ANAZO FUNGUO
ZA UTENDAJI MBINGUNI NA DUNIANI.
2. FUNGUO NI UAMUZI WA
MWISHO WA KUZUIA AU KUACHILIA
Yesu alisema anazo funguo za mauti na
za kuzimu (Ufunuo 1:18).
3. FUNGUO NI UTAWALA
“Na
ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka bagani mwake, yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala
hapana atakayefungua.” (Isaya 22:22)
II. Tumepewa Funguo za
Ufalme
A. Petro Alipewa Funguo
Hizo, “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na
lolote litakalofunguliwa duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.” (Mathayo 16:19).
B. Kanisa zima tuna
Funguo hizo, “Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga
duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani
yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” (Mathayo
18:18). Sema tafsiri zifuatazo apo
chini:
Tafsiri 1
Yesu anauwezo wa
kufanya jambo bila mpaka mbinguni, duniani, kwa mauti na kuzimu
Yesu anauwezo wa
kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Yesu Anao utawala wote,
mbinguni Duniani na kuzimu
Tafsiri 2
Kanisa katika Yesu linauwezo wa kufanya jambo bila
mpaka mbinguni, duniani, na kuzimu
Kanisa katika Yesu
linauwezo wa kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Kanisa katika Yesu
linao utawala wote, mbinguni Duniani na kuzimu
Tafsiri 3
Mimi katika Yesu nina
uwezo wa kufanya jambo bila mpaka mbinguni, duniani, kwa mauti na kuzimu
Mimi katika Yesu uwezo
wa kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Mimi katika Yesu
ninao utawala wote, mbinguni Duniani na
kuzimu
Namna ya Kushika Funguo
1. Tunashika
funguo kwa ufunuo Yesu ni nani, Amefanya
nini, Yupo wapi (Mathayo 16:17-18)
2.Tunapopata marifa ya Neno katika Roho (Luka 11:52,
Waefeso 1’17-18)
3.Tunapozidi kuufahamu moyo wa Mungu sasa tunapoomba,
anataka nini kitokee duniani huko mbinguni. Anaona nini mbinguni moyoni mwake.
Tukijua nakutamka aonavyo mbinguni tukiwa hapa duniani hizo ni funguo za
kufungua yasiyowezekana.
GOD BLESS YOU
ReplyDelete