Thursday, April 30, 2015

FUNGUO ZA UFALME



UNAZO FUNGUO
I. Unaona nini katika Maandiko haya kuhusu funguo
A. Ufunuo 1:17-18, “…Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele, nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu
B.Ufunuo 3:7, “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”.
C. Ufunuo 3:8, Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.”
D. Ufunuo 20:1-3, Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, Ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu.
E. Isaya 22:22, Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka bagani mwake, yeye atafungua  wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.
1. FUNGUO NI UWEZO WA KUFANYA JAMBO BILA MIPAKA
Yesu  alisema amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani(Mathayo 28:18:), Tafsiri yake nyingine anao uwezo wa kutenda mbinguni na duniani. ANAZO FUNGUO ZA UTENDAJI MBINGUNI NA DUNIANI.
2. FUNGUO NI UAMUZI WA MWISHO WA KUZUIA AU KUACHILIA
Yesu alisema anazo funguo za mauti na za kuzimu (Ufunuo 1:18).
3. FUNGUO NI UTAWALA
Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka bagani mwake, yeye atafungua  wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.  (Isaya 22:22)
II. Tumepewa Funguo za Ufalme
A. Petro Alipewa Funguo Hizo, Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote litakalofunguliwa duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.(Mathayo 16:19).
B. Kanisa zima tuna Funguo hizo, Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.(Mathayo 18:18).  Sema tafsiri zifuatazo apo chini:
Tafsiri 1
Yesu anauwezo wa kufanya jambo bila mpaka mbinguni, duniani, kwa mauti na kuzimu
Yesu anauwezo wa kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Yesu Anao utawala wote, mbinguni Duniani na kuzimu
Tafsiri 2
Kanisa  katika Yesu linauwezo wa kufanya jambo bila mpaka mbinguni, duniani, na kuzimu
Kanisa katika Yesu linauwezo wa kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Kanisa katika Yesu linao utawala wote, mbinguni Duniani na kuzimu
Tafsiri 3
Mimi katika Yesu nina uwezo wa kufanya jambo bila mpaka mbinguni, duniani, kwa mauti na kuzimu
Mimi katika Yesu uwezo wa kuzuia, au kuachilia jambo lolote, mbinguni, duniani au kuzimu
Mimi katika Yesu ninao  utawala wote, mbinguni Duniani na kuzimu
Namna ya Kushika Funguo
1. Tunashika funguo kwa  ufunuo Yesu ni nani, Amefanya nini, Yupo wapi (Mathayo 16:17-18)
2.Tunapopata  marifa ya Neno katika Roho (Luka 11:52, Waefeso 1’17-18)
3.Tunapozidi  kuufahamu moyo wa Mungu sasa tunapoomba, anataka nini kitokee duniani huko mbinguni. Anaona nini mbinguni moyoni mwake. Tukijua nakutamka aonavyo mbinguni tukiwa hapa duniani hizo ni funguo za kufungua yasiyowezekana.

1 comment: