Tuesday, February 10, 2015

Usizuiliwe kwa kufikiri



Kufikiria Kunazuia
(Reasoning Limits)
Mungu hajatuzuia kutumia fikra zetu ametuumba nazo, Ila zinapaswa kufanywa upya zisiwe ni kikwazo cha kushirikiana naye (Warumi 12:1-2).
Si kila kitu cha kufikiria, visivyowezekana hatutakiwi kufikiria tunatakiwa kuamini.
Fikira zinafanya kazi na muda, mazingira na uzoefu hali ilivyo au tuseme hali ikoje kwa watu wote. Kwa kwa mfano kwa watu wote huwezi kupata kazi bila usaili, ila kwa Mungu unaweza kupata bila usaili.
MIFANO YA FIKIRA ZILIVYOKUWA KIKWAZO
1. Sina Mtu (Yohana 5:1-8)
A. Yesu alimuuliza mtu huyu, “Wataka kuwa mzima?” Ilipasa kujibu ndio au hapana. Yeye alisema hana mtu wa kumtumbukiza katika birika la maji ili apone, hiki kilikuwa ni kikwazo, kufikiria hivi.
B. Yesu alitenda kinyume na fikra zake, “Inuka Jitwike godoro uende”
TENDO:Jitwike Godoro
2. Najua Atafufuka (Yohana 11:24)
A. Yesu alimwambia Matha ndugu yake atafufuka
B. Katika fikra zake Matha alijua atafufuka siku ya mwisho, Pia ananuka ameshakufa siku nne (11:39), Msitari wa 21 na 22 inaonyesha pia alikuwa na anajua kwamba Yesu akiomba Mungu atajibu (Mental agreement not faith), maana mbele alianza kusema ananuka na atafufuka siku ya mwisho.
C. Yesu hapohapo akasema yeye ni ufufuo na uzima, Pia akiamini ataona utukufu (11:25, 11:40)
TENDO: Liondoeni Jiwe (11:39-41)
3. Lakini Hivi ni Nini kwa Watu Wengi kama Hawa? (Yohana 6:1-9)
A. Yupo mtoto hapa na samaki wawili na mikate mitano
B. Hivi ni nini (fikira zinakataa)
TENDO: Waketisheni chini (10), Akashukuru, Wagawieni(11), (Inawezekana aliposhukuru iliongezeka au alipoanza kugawa).
4. Tumefanya kazi ya Kuchosha (Luka 5:1-5)
A. Alisema tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha.
B. Hapo hapo akabadilisha na kuingia rohoni, lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
-Tubadilike haraka kutoka katika kufikiria kwenda katika imani
TENDO: Tweka mpaka kilindini
5. Mimi ni mzee na mke wangu Ana umri mkubwa (Luka 1:18)
A. Zakaria na Elizabeti walikuwa ni wenye haki (Msitari 6)
B.Elizabeti alikuwa tasa (Msitari 7)
C. Malaika aliwatokea (Msitari 11)
D. Malaika alimwambia Zakaria maombi yake yamesikiwa, atapata mtoto wa kiume na atakuwa na furaha (Zekaria)
E. Atajazwa Roho toka tumboni, atakuwa mkuu, atakuwa na roho ya Elia
Fikra za kuangalia muda na mazingira zilizuia yote haya (Msitari 18).
6.Mbwa Wanakula makombo mezani mwa Bwana zao (Marko 8:24-28)
A. Mwanamke huyu alikataa fikira kumwekea mpaka
B. Sababu za kufikirika za kumfanya asipokee zilikuwepo
1.Ilipaswa watoto washibe kwanza
2.Sio sawa uponyaji wa watoto wapewe mbwa
Hakukubali fikra hizi zimzuie.
7.  Basi akaenda na kunawa akarudi anaona (Marko 9:1-7)
A. Yesu alitema mate chini, akatengeneza tope (none sense)
B. Akampaka kipofu machoni
TENDO: Nenda kanawe (Siloamu)
C. Mtu huyu hakufikiri kabla ya kutenda alitenda tu!
D. Viongozi wa Kiyahudi walifungwa na fikira (9:24-25)
E. Aliwajibu viongozi wa Kiyahudi, mimi sijui ana dhambi au la (au alitumia matope) mimi najua nilikuwa mgonjwa na sasa naona.
Tunahitaji Neno na Roho Mtakatifu

No comments:

Post a Comment