Saturday, February 28, 2015

Mungu Pamoja Nasi



IMANUEL
(Mathayo 1:23)
Kusudi la mtu au mwisho wake , au  mustakbali wake unaweza kuonekana kwa vitu visivyopungua viwili
1.Unabii Ulionenwa juu yake
2.Jina lake au majina yake
Jina la Imanueli ambalo pia ni jina la Yesu laonyesha kusudi moja la Yesu alilokuja kutimiza duniani. Andiko hilo hapo juu linasema, ataitwa Imanueli yaani Mungu pamoja na wanadamu. Kuja kwa Yesu ni mlango wa Mungu kukaa na wanadamu.
A. Anakaa Nasi kwa Njia ya kuzishika Amri Zake(Yohana 14:21,23)
1. Kuliamini jina la Yesu (1Yohana 3:23): Amri hii ya kuliamini jina lake, tunaanza kuitii tunapompokea Yesu kama Mwokozi. Tumapoitii Yesu anaanza kukaa nasi kwa uzima wake (1Yohana 5:13).
2.Kupendana sisi kwa sisi (1Yohana 3:23).
B. Anakaa Nasi kwa Roho wake Mtakatifu (1 Yohana 3:24)
Roho Mtakatifu ni chanzo cha makao ya Mungu pamoja nasi. Miili yetu ni hekalu la Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu (1Wakorintho 3:16, 6:19-20). Mungu anasema atakaa ndani yetu na kati yetu atatembea (2 Wakorintho 6:16). Siku ya leo wakati ninaomba nilipata ushuhuda moyoni usemao, “Roho Mtakatifu ni Imanueli”. Yesu ni Imanueli, Roho pia analo jina hilo maana ni mmoja na Yesu.
C. Anakaa Nasi Mkono wa Kuume (Waefeso 2:5-6)
Yesu ni Mungu pamoja nasi mkono wa kuume wa Mungu. Yuko pamoja nasi juu ya kila jina, nguvu au mamlaka. Tunamwakilisha duniani toka mkono wa kuume mbinguni. Mkono wa kuume tunatawaka pamoja naye kama wafalme na makuhani. Tuko pamoja naye kama kuhani wetu na mwombezi wetu.
D. Atakaa Nasi Milele (Ufunuo 21:3)
Mungu atafanya maskani yake na sisi milele. Yeye atakuwa ni  hekalu na sisi tutakuwa ni watu wake tulio ndani yake.
JINA LA IMMANUEL NI JINA LA KINABII LA MUNGU KUKAA NASI. MUNGU ANAPENDA KUKAA  NA WATU, ANAKAA NASI KWA NJIA YA YESU KRISTO, IMMANUEL MUNGU PAMOJA NA WANADAMU. HAPA NINAPOANDIKA IKIWA UMEMPA YESU MAISHA YAKO MUNGU YUPO NA WEWE! UNAYO ROHO YAKE, UZIMA WAKE NA SAUTI YAKE KATIKA UFAHAMU WA ROHONI. KATIKA KIPINDI HIKI MSHUKURU MUNGU KWA KUKAA NA WEWE KWA NJIA YA YESU.

No comments:

Post a Comment