Hautoki Mkononi Mwake
“Wote anipao Baba watakuja kwangu; Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa
nje kamwe”
(Yohana 6:37)
Ikiwa umempa Yesu maisha yako,
Mungu Baba amempa Yesu maisha yako. Ulipokwenda kwa Yesu na kumwamini, haikuwa
wewe ilikuwa ni Mungu Baba anakupeleka kwa Yesu. Andiko lingine linasema, “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa
na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. Imeandikwa katika
manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na
kujifunza kwa Baba huja kwangu.” (Yohana 6:44-45).
Baada ya Yesu kukupa ufunuo
ukamfahamu Yesu moyoni na kwenda kwake, Yesu anasema hakuna mtu awezaye kukutoa
katika mikono yake Yesu.
Hakuna pepo, Shetani, jaribu,
shida, malaika au kitu kingine chochote, kiwezacho kukutoa katika mikono ya
Yesu. Kwa kuwa upo mikononi mwa Yesu upo salama. Fikiria hivyo, sema hivyo,
waza hivyo.
Hakuna kitu kiwezacho
kukutoa katika mikono ya Yesu, upo salama. HAUTOKI MIKONONI MWAKE.
No comments:
Post a Comment