Yote Yanawezekana
Namshukuru Mungu kwa kutupa faraja ya maandiko yanayoonyesha
kwamba yote yanawezekana kwake. Leo nimetafuta mistari michache ambayo naamini
itaijenga imani yako ikiwa utaisoma na kuitafakari. Isome, irudie rudie na
kuisema ,kisha utaanza kuona moyoni Mungu anaweza yote.
1. Mwanzo 18:14
Mungu alionyesha kwa Sara hakuna neno la kumshinda, atapata
mtoto.
2.Yeremia 32:27
Mungu aliuliza kuna neno gani gumu la kumshinda? Kwa wenye
mwili.
3.Ayubu 42:2
Ayubu alimsema Mungu kwamba anaweza yote na makusudi yake
hayazuiliki.
4.Mathayo 3:9
Yohana mbatizaji alionyesha Mungu anao uwezo wa kugeuza mawe
yawe watoto wa Ibrahim! Hii yaonyesha anaweza yote.
5.Warumi 4:21
Ibrahimu alijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale
aliyoahidi.
6.Luka 1:37
Malaika alisema hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu,
akimaanisha, hakuna ahadi ya Mungu isiyo na nguvu ya kujitimiza au kutimia.
7.Mathayo 19:26
Yesu alisema yote yawezekana kwa Mungu!
8.Yohana 15:5
Yesu alisema pasipo yeye hatuwezi lolote, kwa hiyo pamoja
naye tunaweza yote.
9.Luka 17:20-21
Yesu alisema tukiwa na imani kama chembe ya haradali, imani
inayokuwa na kusema tunaweza kuamisha mlima wala hakutakuwa na jambo
lisilowezekana kwetu. Imani hii hutokea katika maombi na kufunga.
10.Marko 9:23
Yesu alisema yote yawezekana kwa aaminiye, Yote yawezekama
kwa mtu aiwekaye imani yake kwa Mungu awezaye yote, anaanza kuweza kama Mungu
awezavyo.
11. Marko 14:36
Yesu kabla hajasulubiwa wakati anaomba alisema Aba Baba yote
yanawezekana kwako.
Unaweza Pamoja na Mungu
No comments:
Post a Comment