Katika somo hili fupi utaenda
kujifunza njia kadhaa atumiazo adui Shetani kuzuia uungu na kudumisha
‘ushetani’ katika maisha ya mtu au watu. Kuzifahamu mbinu zake (fikra zake)
kunakupa uwezo wa kumpinga na kumzuia, hatimaye kuona mpango wa Mungu
unadhihirika, hatukosi kuzijua fikra zake (2Wakorintho 2:11).
1. Anazuia (1 Wathesalonike 2:18)
Unapomuombea mtumishi au huduma
mpinge Shetani asizuie shauri la kiungu kupitia mtumishi huyou huduma hiyo.
2. Anapotosha (2 Timoteo 4:1)
Kuna roho maalum ambazo kazi yake
ni kupotosha mtu wa Mungu asifuate kweli. Hizi hufanya kazi katika fikra na
mawazo. Kushindwa kwake ni kwa njia ya kujifunza neno la Mungu wakati wote, na
kufanya maombezi katika fikra na mawazo ili kulindwa kwa damu ya Yesu, hasa
kama mtu ni mchanga.
3. Anachelewesha (Danieli 10:13)
Mkuu wa Uajemi (Pepo)
alichelewesha Danieli asipate majibu ya maombi yake. Mpaka pale malaika Mikaeli
alipotumwa kumsaidia malaika Gabrieli kupeleka majibu kwa Danieli.
4. Anachochea (Matendo 16:17-22)
Hapa Shetani aliwachochea watu, ili
Paulo na Sila wapate matatizo. Pepo waliyemkemea inawezekana alikuwa mkuu wa
giza aliyeleta uchochezi huo katika watu wanaoonekana.
5. Anazingira (Ayubu 1:13-17)
Alimzingira Ayubu kwa mnyororo wa
matatizo ili akufuru. Ayubu alishinda kwa kukaza macho yake kwa Mungu.
6. Anapooza (1 Samweli 17:10-11)
Wana wa Israeli walitokewa na
Goliati na hawakuweza kufanya chochote walipooza. Mara nyingine adui huleta
matatizo makubwa na kumpoozesha mtu kwa woga. Hapa litazame tatizo kwa kulipima
na ukuu wa Mungu kisha lisemeshe kama Daudi alivyomsemesha Goliati.
7.Analazimisha (Marko 5:1-6)
Hapa mtu huyu alikuwa na pepo
waliomlazimisha kufanya asiyoyataka na asiyo weza. Alikaa makaburini, alivunja
minyororo nk. Shetani alimlazimisha Roho wa Mungu halazimishi, anashauri na
kuhamasisha sio kulazimisha. Dalili za utandaji wa pepo ni mtu kufanya kwa
nguvu vitu asivyotaka kufanya, au mtu kulazimisha mtu mwingine afanye jambo
hasa kama ni baya. Mtu wa namna hii inawezekana anaongozwa na pepo.
8. Anapofusha (2 Wakorinto 4:4)
Kwa watu wasiookoka Shetani
anawapofusha katika fikra zao wasielewe injili, Kisha wafe katika dhambi zao.
Maombi ya kuwaombea ni kufunga giza la kishetani na kufungulia nuru ya Kristo
waelewe injili. Kwa mtu aliyeokoka na anadumu kuendelea na dhambi atafanywa
moyo mgumu na kupofushwa. Mwishowe hataweza
kutubu na atapotea milele.
HII NI BAADHI YA
MIKAKATI TU YA ADUI. TUNAWEZA KUMZUIA KWA JINA LA YESU,
DAMU YAKE NA NENO LA MUNGU.
No comments:
Post a Comment