HATI MILIKI YA YESU
Jina la Yesu ni kama hati miliki
ya kummiliki Yesu na kazi zake hapa duniani. Kazi ya hati ni kutoa haki na
uwezo wa kumiliki ardhi, nyumba nk. Jina la Yesu limetupa uwezo sisi waumini wa
kuzimiliki kazi zote alizozifanya Yesu! Pia kuwa na Yesu sasa.
Kichwa, Mwili,
Matendo
(Waefeso 1:22-2)
Yesu ni kichwa cha kanisa, kanisa
ni mwili wake. Mwili huwa unayo matendo fulani, mwili wa Yesu unayo matendo
yake. Unayatenda matendo hayo kwa kutumia jina la Yesu. Kwa jina la Yesu kanisa
limemiliki hali ya Yesu aliyonayo mkono wa kuume wa Mungu. Yuko juu ya nguvu na
mamlaka zote. Udhihirisho wa hali hiyo ya nguvu na mamlaka unaonekana kwa
kupitia kanisa hapa duniani kwa jina lake.
Mambo Tunayomiliki
kwa Jina lake
1. Kwa jina la Yesu tunamiliki
Wokovu (usalama wa milele), (Matendo
2:21).
2. Kwa jina la Yesu tunamilliki
uponyaji (Yoeli 2:32).
3.Kwa jina la Yesu tunaingia
patakatifu pa patakatifu kwa njia ya kuomba kwa jina lake. Huku ni kuomba kwa
kumtumia Yesu (Yohana 16:23).
4.Kwa jina la Yesu tunatenda kama
alivyotenda na kazi kubwa zaidi (Yohana 14:12-13).
5.Kwa jina la Yesu tunatoa pepo
kama alivyotoa (Marko 16:17).
6. Kwa jina la Yesu
tumemilikishwa uwezo na mamlaka ya kuwa juu ya vyote kama Yesu alivyo (Yohana
3:35, Mathayo 11:27, Mathayo 28:18).
7. Kwa jina la Yesu tunao uwezo
wa kuingia popote na kuamuru jambo litokee hata kama tuko mbali kimwili (1
Wakorintho 5:3-4).
ASANTE BABA KWA KUTUMILIKISHA
YESU NA KAZI ZAKE KWA JINA LAKE
No comments:
Post a Comment