Monday, January 12, 2015



FUNGUO ZA UFALME

Ufalme wa Mungu unaonekana kwa tabia za Mungu, pia nguvu na mamlaka yake. Funguo ni ishara ya mamlaka na nguvu za Mungu. 

I.            FUNGUO
Maphteah (Kiebrania) – kifungulia      (Opener)
Waamuzi 3:25Wakamngoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa.
Kleis (Kiyunani)  - Kufunga
Luka 11:52Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.

II.         Funguo ni Mamlaka na nguvu (Alama ya mamlaka na nguvu)


MAENENO ZINAPOONEKANA KIMAANDIKO

1. Begani.       Isaya 22:22Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.
·       Inaonyesha mtawala aliye katika ofisi yenye mamlaka. Ofisi hii ni ya Kristo.
·       Kristo ana uweza wa kifalme begani (funguo za kifalme)

2. Petro
·       Yesu alimwambia Petro amempa funguo za Ufalme. Mathayo 16:19Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
·       Mamlaka na nguvu ya kifalme

3. Yesu
·       Anazo funguo za mauti na za kuzimu. Ufunuo 1:18na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai; nami hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
·       Anazo funguo za Daudi. Ufunuo 3:7Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
·       Mamlaka na nguvu ya ufalme.

4. Malaika.
·       Ufunuo 9:1Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.
·       Ufunuo 20:1 - 2 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. (2) Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu “

5. Maarifa
·       Ufunguo wa ufalme
·       Kuyashiriki mambo ya kifalme, maarifa ni uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo.
Luka 11:52Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa  
maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
·       Mathayo 23:13Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.

SIKU MOJA WAKATI NAOMBA ASUBUHI NILIFAHAMU KWAMBA:

1.  FUNGUO NI MAMLAKA YA KUTENDA.

Ufunuo 1:18na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai; nami hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
      
Maandiko haya yanaonyesha:

-      Yesu anazofunguo za mauti na za kuzimu, anayo mamlaka ya kudhibiti, mauti na kuzimu.

-      Mikononi mwake ameshika mamlaka yote ya utendaji wa mauti (nguvu) na kuzimu (viumbe vya kuzimu).

-      “Control” ya utendaji wa mauti na kuzimu ipo chini yake

-      Maamuzi ya mashetani juu ya watu ameyashika na kuyazuia

-      Hawawezi kufanya watakavyo tena

2.  FUNGUO NI UFUNUO WA KIROHO

Mathayo 16:16 – 19Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. (17) Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Baryona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. (18) Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. (19) Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

· Petro alipopata ufunuo Yesu ni nani, Yesu akataja funguo

· Tupatapo ufunuo, tayari tuna funguo, Maarifa ni funguo. Luka 11:52Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.

                          RHEMA NI FUNGUO

·       Rhema katika maombezi
·       Rhema katika mahubiri
·       Rhema katika maisha

3.  UWEZO WA KUZUIA NA KUACHILIA

Ufunuo 3:7Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

Yesu anafungua (Anaruhusu) wala hapana azuiaye. Anazuia (Anafunga) wala hapana anayeruhusu.

·       Kwa kutumia jina lake tunauwezo wa kuruhusu na kuzuia vitu. Marko 16:17 “ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;”

·       Kwa nafsi yake tuna uwezo wa kuruhusu na kuzuia vitu. Yohana 14:30Mimi sitasema nanyi  maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

·       Kwa Neno lake tuna uwezo wa kuruhusu na kuzuia vitu Yohana 8:51Amin, amin, nawaambia, mtu akilishika Neno langu, hataona mauti milele.

·       Kwa damu yake yake tuna uwezo wa kuruhusu na kuzuia vitu. Ufunuo 12:11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neon la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

·       Kwa Roho wake tuna uwezo wa kuruhusu na kuzuia vitu. Isaya 59:19 “

UNAZO FUNGUO KATIKA KRISTO
Soma Maandiko haya
1.  1Petro 3:22 “Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.

2.  Yohana 3:35 “Baba amempenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

3.  Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

4.  Mathayo 11:27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

5.  Yohana 10:17 – 18 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. (18) Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.”

6.  Yohana 10:30 “Mimi na Baba tu umoja.

7.  Yohana 1:18 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

8.  Yohana 8:58 “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

9.  Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

10.      1Petro 2:6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatataharika.”

MAMLAKA YA KUTENDA YA SHETANI YESU AMEISHIKA
-      MAUTI (Nguvu)
-      KUZIMU (Mashetani)
INATHIBITIKA KWAKO
-      KWA JINA LAKE
-      KWA NENO LAKE
-      KWA ROHO WAKE
-      KWA DAMU YAKE
-      KWA NAFSI YAKE

No comments:

Post a Comment