Wednesday, January 7, 2015

Ni Sisi Anatutegemea


UNAYO MAMLAKA
Katika maandiko usomapo, hasa Agano jipya utagundua kwamba sisi ndiyo tunayo mamlaka ya kumshughulikia Shetani na sio Mungu. Mungu ametupa mamlaka sisi. Katika maandiko yafuatayo utaona wajibu upo kwetu ili kumshughulikia Shetani, Mungu anatenda kupitia sisi:

1. Mtiini Mungu, Mpingeni Shetani naye atakimbia (Yakobo 4:7)
Andiko hili linaonyesha ni sisi tunaompinga Shetani. Wajibu wa kumpinga na kumfukuza ni wetu!
2. Nawapa amri, Kukanyaga nyoka na nnge na nguvu zote za yule mwovu (Luka 10:19)
Ni sisi waamini ndio tunao wajibu wa kukanyaga nyoka na nnge na nguvu zote za Shetani wala hakuna kitu kitakachotudhuru.
3. Lolote mtakalolifunga duniani litafungwa na mbinguni (Mathayo 18:18-19)
Uwezo wa kufunga jambo au kufungua upo katika mikono yetu.
4.Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, enendeni (Mathayo 28:18-19).
Yesu amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, kwa mamlaka hiyo aliyo nayo sisi tunaenda duniani kufanya jambo siyo yeye.
5. Na Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo (Marko 16:17-18).
Uwezo wa kutoa  pepo ni wetu, Ni sisi tunaotoa pepo kwa kutumia jina alilopewa Yesu, lililobeba mamlaka yake yote.
MAANDIKO YANASEMA YESU AMEFANYWA KICHWA JUU YA VYOTE KWAAJILI YA KANISA (WAEFESO 1:22-23), SIYO KWAAJILI YAKE. AMEWEKWA JUU YA VYOTE KWAAJILI YETU, ILI SISI TUWEZE KUFANYA JAMBO FULANI BADALA YAKE KAMA WAWAKILISHI WAKE.

No comments:

Post a Comment